LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Haya ndio Matokeo ya Chelsea,Arsenal,Man City Mechi za ligi ya EPL October 18, 2014. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, October 19, 2014

LIGI KUU UINGEREZA 2014/2015:-Haya ndio Matokeo ya Chelsea,Arsenal,Man City Mechi za ligi ya EPL October 18, 2014.

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Uingereza, Manchester City wakicheza kwao Etihad wameichapa Tottenham Bao 4-1 katika Mechi ya Ligi Kuu na Bao zote kufungwa na Straika wao wa Argentina Sergio Aguero ambae pia alikosa Penati moja huku nao Spurs wakikosa Penati iliyopigwa na Roberto Soldado.

Mara baada ya Mechi, Meneja wa Man City, Manuel Pellegrini, amefananisha umuhimu wa Aguero kama ule wa Cristiano Ronaldo kwa Real Madrid na Lionel Messi kwa Barcelona.


Vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, wameendelea kubembea kileleni baada ya kushinda Ugenini walipoichapa Crystal Palace Bao 2-1 wakati Uwanja wa Emirates ulihitaji Bao la Dakika za Majeruhi la Danny Welbeck kuipa Sare Timu ya Nyumbani Arsenal na Southampton, wakicheza kwao, kuifumua Sunderland Bao 8-0 hapo jana October 18, 2014,kwenye mechi za Ligi hiyo.

Chelsea walishinda Mechi yao  kwa Bao za Oscar, Dakika ya 6, na Cesc Fabregas, Dakika ya 51, na Palace kufunga Bao lao Dakika ya 90 kupitia Fraizer Campbell.

Kila Timu ilimaliza ikiwa Mtu 10 baada ya Beki wa Chelsea Cesar Azpilicueta kupewa Kadi Nyekundu Dakika ya 40 na Mchezaji wa Palace Damien Delaney kutolewa Dakika ya 43.
Huko Emirates, Alexis Sanchez aliifungia Bao Arsenal Dakika ya 13 na Mohamed Diame kuisawazisha Hull City Dakika ya 17 na kisha Abel Hernandez kuipa uongozi Dakika ya 46.

Lakini, Danny Welbeck, Mchezaji wa zamani wa Man United, aliikatili Hull City inayoongozwa na Meneja Steve Bruce, Nahodha wa zamani wa Man United, kwenye Dakika za Majeruhi kwa kusawazisha.

Sanchez, left, has scored six in all competitions since signing from FC Barcelona
Nao Southampton wameisambaratisha Sunderland kwa Bao 8-0 kwa Bao za kujifungwa wenyewe za Santiago Vergini na Liam Bridcutt, Graziano Pelle, Bao 2, Jack Cork, Dusan Tadic, Victor Wanyama na Sadio Mane.

As It Stands Table EPL 2014/2015.


Position Team Played Goal Difference Points
Karibu kwenye familia ya Makonda Blog na uzipokee Picha/Habari zote kwa kutumiwa Mchana /Usiku baada tu ya kujiunga kwa kubonyeza hapa mtu wangu >>>BONYEZA HAPA.>>>Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.
No Movement 1 Chelsea 8 15 22
No Movement 2 Man City 8 10 17
No Movement 3 Southampton 8 14 16
Moving up 4 West Ham 8 4 13
Moving down 5 Man Utd 7 3 11
Moving up 6 Arsenal 8 2 11
Moving down 7 Swansea 7 2 11
Moving down 8 Tottenham 8 -1 11
Moving up 9 Hull 8 0 10
Moving down 10 Liverpool 7 0 10
Moving down 11 Aston Villa 8 -8 10
Moving up 12 Everton 8 0 9
Moving down 13 Leicester 8 -2 9
No Movement 14 West Brom 7 -1 8
Moving up 15 Stoke 7 -2 8
Moving down 16 Crystal Palace 8 -3 8
Moving down 17 Sunderland 8 -7 8
No Movement 18 Newcastle 8 -6 7
No Movement 19 Burnley 8 -9 4
No Movement 20 QPR 7 -11 4


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad