![]() |
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo April 5,
2018 ametuma salamu za rambirambi kufuatia ajali iliyotokea katika
Kijiji cha Makomero, Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Jana April 4, 2018
saa 2:00 usiku na kusababisha vifo vya watu 12.
“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa
taarifa ya vifo vya watu 12 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani
iliyotokea jana usiku katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora, nawapa pole wafiwa
wote, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu mkubwa.” -JPM
|
![]() |
|
Ajali hiyo
imetokea baada ya basi la kampuni ya City Boy lililokuwa limebeba abiria kutoka
Karagwe Mkoani Kagera kuelekea DSM kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso
lililokuwa linatoka Singida kuelekea Igunga.
Pamoja na
kutoa pole kwa wafiwa na kutoa maelekezo hayo, Rais Magufuli amewataka viongozi
wote wanaohusika na usimamizi wa usalama wa barabarani kutafakari kwa nini
ajali nyingi zimekuwa zikitokea katika maeneo yaleyale na kutafuta ufumbuzi ili
kuepusha madhara ya watu kupoteza maisha, kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza
mali.
Rais
Magufuli amemtaka
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri kufikisha salamu zake za pole kwa
wafiwa wote, na amewaombea Marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi na
majeruhi wote 46 wapone haraka ili waungane na familia zao katika ujenzi wa
Taifa.
|







No comments:
Post a Comment