Saturday, August 27, 2016

NEW
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Meja Jenerali Salum M.Kijuu katika kuteleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa tarehe 29/04/2009 linalomtaka kuzisimamia Halmashauri za Wilaya kila moja kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali baada ya kupokelewa kwa taarifa hiyo, Mkuu wa Mkoa  tayari ameagiza kuchukuliwa hatua kwa watendaji 8 waliohusika na uzembe na upotevu wa fedha za Serikali katika Halmashauri mbili za Wilaya alizopitia kusimamia zoezi hilo.

Mhe. Kijuu tayari amesimamia zoezi la kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Halmashauri za Wilaya ya Bukoba Muleba na Ngara ambapo katika zoezi hilo  aliagiza hatua kuchukuliwa mara moja kwa Watendaji saba Katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba na Mtendaji mmoja katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Atumbua Jipu Watumishi Wanane wa Halmashauri Bukoba na Ngara kwa Ubadhirifu wa Fedha za Serikali.

Read More

Msimamo wa Ligi kuu soka Vodacom Tanzania bara 2016/2017 baada ya mechi za ufunguzi wikiendi.

Ratiba ya Mnyukano Viwanjani wikiend hii Ligi kuu Vodacom Tanzania bara 2016.

Read More

Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kwenye nyumba iliyo eneo la Vikindu wilayani Mkuranga.

Taarifa ambazo zimepatikana kutoka kwa watu waliokuwa karibu na operesheni hiyo na ambazo hazijathibitishwa na mamlaka rasmi, zinasema kamishna wa Kitengo cha Kuzuia Ujambazi, ASP Thomas Njuki aliuawa kwa kupigwa risasi kichwani.

Taarifa hizo zilisema kuwa jambazi mmoja aliuawa ingawa idadi ya waliokamatwa haikufahamika mara moja kutokana na mashuhuda kutoa takwimu tofauti.

Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema ataongea na waandishi wa habari leo saa 4:00 asubuhi kuzungumzia tukio hilo.

Tukio hilo limetokea siku chache baada ya askari wanne wa Jeshi la Polisi kuuawa wakati wakibadilishana lindo kwenye tawi la benki ya CRDB lililoko Mbande jijini Dar es Salaam.

Nyumba waliokuwa Wanaishi hao Majambazi.

Watu hao, waliofika wakiwa wamepanda pikipiki, walipora silaha na kutoweka nazo. Katika tukio la jana, askari wa Jeshi la Polisi walikuwa na nia ya kuwakamata watu waliowashuku kuwa ni majambazi.

Kwa mujibu wa watu wanaoishi karibu na nyumba hiyo, mpambano kati ya polisi na majambazi hao ulianza saa 7:30 usiku baada ya polisi kuvamia nyumba walimopanga majambazi hayo.

Tukio lilivyotokea.

Chanzo kimoja cha habari kimeeleza kuwa baada ya polisi kufuatilia nyendo za wakazi wa nyumba hiyo walianza upelelezi na kubaini kuwa huenda wanahusika na matukio kadhaa ya uhalifu, likiwamo la uvamizi wa kituo cha polisi cha Stakishari na lile la tawi la CRDB Mbande mkoani Pwani.

Mpashaji huyo alisema kuwa jana saa saba usiku, polisi walifika kwenye nyumba hiyo iliyo Mtaa wa Vikindu Mashariki ambayo ina maduka upande wa mbele, ikipakana na nyumbani nyingine mbili pembeni na nyuma zikiwa umbali usiozidi hatua nne.

Habari hizo zinasema askari hao kwanza walimtuma mwenyekiti wa serikali ya mtaa kwenda kuwasihi wafungue mlango na walipokataa ndipo walipoenda kugonga, wakiwaamrisha watu hao wafungue mlango.

Baada ya kuona hawatii amri ya kufungua mlango, polisi waliamua kuvunja vitasa kwa kutumia bastola, ndipo risasi zikaanza kurushwa,” alisema mpashaji habari huyo.

 Kwa kuwa mkuu alikuwa mbele, wahalifu walimpiga risasi kichwani na alikufa palepale.”
Mtu huyo alisema kuwa baada ya Kamishna Njuki kufariki, askari wengine walirudi nyuma kujihami zaidi.

Baada ya hapo polisi waliendelea kupiga risasi kuelekea maeneo mbalimbali ya nyumba hiyo na wahalifu hao kujibu mashambulizi.

Kila chumba ambacho polisi walikuwa wakijaribu kurusha risasi, zilijibiwa. Inaelekea kila chumba kilikuwa na mtu mwenye silaha,” alisema shuhuda mwingine wa tukio hilo.

Habari kutoka kwa majirani zinasema hadi saa 2:45 asubuhi, milio ya risasi iliendelea kurindima katika eneo hilo.

Baadaye polisi waliomba kuongezewa nguvu na Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao walifika na kuendeleza mapambano hayo.

 Mtoto ataja alipojificha baba.

Wakati mapambano yakiendelea, sauti za watoto waliokuwa wakilia zilisikika na ndipo askari wa JWTZ waliamuru watu hao wawatoe nje.

Watoto walipotoka nje, polisi waliwauliza baba yupo wapi, mtoto mmoja akajibu yupo darini,” alisema

Baada ya polisi kusikia hivyo, walielekeza mashambulizi yao darini na kufanikiwa kumjeruhi mtu aliyejificha darini ambaye alishuka.

Wakati polisi wakishinikiza atoke ndani ili kujisalimisha, mtu huyo alijipiga risasi mara baada ya kutoka na kufariki dunia.
Wakazi Vikindu wahaha!

Kutokana na tukio hilo, taharuki ilitanda kwa wakazi wa Vikindu na biashara zote zilifungwa eneo hilo huku wananchi wakiwa na chupa za maji kutokana na mabomu ya machozi yaliyokuwa yakipigwa kila mara.

Wakazi wa eneo ambalo lipo karibu na maegesho ya magari ya Farid Seif, hawakuruhusiwa kutoka ndani na waliofanikiwa kutoka usiku hawakuingia hadi jana saa 7.00 mchana wakati hali ilipotulia.

Kutokana na majibizano ya risasi, watu wanaofanya kazi jijini Dar es Salaam ambao wanaishi vijiji vya Melela, Vianzi, Pemba Mnazi na Mfuru hawakwenda kazini kutokana na barabara inayotoka Vikindu kufungwa hadi saa 7.00 mchana.

Tukio hilo lilisababisha umati wa watu kukusanyika kushuhudia mapambano hayo, lakini hakuna raia aliyeruhusiwa kuvuka mita 150 kwenda eneo la tukio.

Polisi Mwingine Auawa katika Mapambano Makali na Majambazi –Mkuranga.

Read More

Kurasa za Habari Katika Magazeti ya Leo Jumamosi Agosti 27,2016.

Read More

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na matamshi ya Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam yanayokiuka misingi ya utawala bora aliyoyatoa tarehe 25 Agosti, 2016 wakati wa kuaga miili ya askari Polisi watatu waliouawa Mbande, Mkoani Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Bahame Tom Nyanduga, leo (Agosti 26, 2016) Mhe. Makonda ametumiwa barua ya wito inayomtaka afike makao makuu ya Tume mtaa wa Luthuli, tarehe 30 Agosti, 2016 ili kujadili kile Tume ilichokiona kuwa ni kejeli kwa Tume pamoja na jumuiya yote ya watetezi wa haki za binadamu.

Paul Makonda aitwa Tume ya Haki za Binadamu Kujieleza kuhusu Polisi Wawapige Watu Wakiwakuta Msituni.

Read More

Friday, August 26, 2016


Madera wa Tanzania wanaoendesha magari ya mizigo kuingia nchini Burundi wamejikuta katika wakati mugumu baada ya kunyanyaswa na askari wa burundi kwa kuwatoza fedha zisizokuwa na stakabadhi ambapo fedha zinapokosekana wanafungiwa  kwenye vyoo.

Magari 36 ya Mizigo Kutoka Tanzania kwenda Burundi yasitisha Huduma kituo cha Forodha Kobero.

Read More

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 Ndugu wanahabari,
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa sana taarifa ya kushambuliwa na kuuawa kwa askari wa jeshi la Polisi wakiwa katika kutekeleza majukumu yao ya ulinzi eneo la Mbande, Temeke jijini Dar Es Salaam.

CCM yaomboleza Vifo Vya Polisi Waliouawa na Majambazi.....na Tamko lao kuhusu Maandamano ya UKUTA.

Read More

Van Persie (kulia) alifunga mabao 58 mechi 105 alizochezea Manchester United

Manchester United watakutana na klabu anayochezea nyota wao wa zamani Robin Van Persie- Fenerbahce- pamoja na Feyenoord na Zorya Luhansk hatua ya makundi Europa League.

Droo Europa League 2016/2017: Man Utd kukutana na Robin van Persie, Mbwana Ally Samatta na Athletic Bilbao.

Read MorePicha Uongozi na Watumishi Radio Kwizera FM wampokea kwa Kishindo Bi.Auleria Gabriel baada ya Kutwaa Tuzo ya Mwandishi Bora wa Masuala ya Jinsia.

Read More


Picha Mkuu wa Mkoa wa Kagera azindua Mpango Mkakati wa Kulinda Raslimali za Uvuvi ili kutokomeza uvuvi haramu.

Read More

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu Akitoa Taarifa ya Mkoa Kwa Waziri Kairuki..Picha na Maktaba yetu.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu awaagiza viongozi katika Halmashauri za Wilaya kuchukukua jukumu la kusimamia kikamilifu shughuli mbalimbali za afya katika  Mkao wa Kagera  ili kuboresha utoaji wa huduma za afya kikamilifu katika jamii.

Kutoingiza takwimu za afya katika mfumo wa Wizara ya Afya , Biharamulo yapata asilimia 0% (sifuri).

Read More

Vijuso Katika Magazeti Leo Ijumaa Agosti 26,2016.

Read More

Thursday, August 25, 2016


Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akiwa Mkoani Kagera aliawaagiza viongozi wa Mkoa kuhakikisha wanaondoa data chafu za Watumishi katika mfumo wa utumishi ili kuondokana tatizo la Watumishi hewa.

Mhe. Kairuki alitoa agizo hilo alipokuwa akiongea na Mkuu wa Mkoa Meja Jenarali Mstaafu Salum M. Kijuu ofisini kwake mara baada ya kuwasili Mkoani hapa kwaajili ya kikao kazi cha kuongea na Watumishi wa Serikali kutoka katika Taasisi na Idara mbalimbali za Serikali Mkoani Kagera.

“Mhe. Mkuu wa Mkoa katika Mkoa wako kuna data chafu kama ifuatavyo, katika Sekretarieti ya Mkoa zipo data chafu 21, Bukoba Manispaa 70, Biharamulo 296, Halmashauri ya Wilaya Bukoba 429, Karagwe 211, Muleba 51, Ngara 454, Missenyi 1,608 na Kyerwa 234.”

 Mhe. Kairuki alitoa takwimu hizo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera na kusistiza data hizo kuondolewa katika mfumo mara moja.

Halmashauri ya Missenyi , Bukoba na Ngara zaongoza kwa Data Chafu mkoani Kagera.

Read More

Copyright ©mwanamakonda 2014 Mwana Wa Makonda | Designed by Lon Technology By lon Templateslon technology