|
Wekundu wa Msimbazi Simba SC imejitanua kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2017/2018 baada
ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Njombe Mji FC jioni ya leo April 3,2018 kwenye uga
wa Saba Saba mjini Njombe.
Pongezi kwa mfungaji wa mabao hayo yote mawili leo, Nahodha John Raphael
Bocco ‘Adebayor’, moja kila kipindi na sasa Wekundi wa Msimbazi wanafikisha
pointi 49 baada ya kucheza mechi 21, wakiwazidi kwa pointi tatu mabingwa
watetezi, Yanga SC wenye pointi 46 za mechi 21 pia.
Katika mchezo huo, Kiungo Haruna Niyonzima na beki Mbonde waliingia kipindi cha
pili wakichukua nafasi za Emmanuel Okwi na James Kotei.
Mbode na Niyonzima
walikosekana dimbani kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi.
MSIMAMO WA LIGI ULIVYO SASA.
|
No comments:
Post a Comment