
![]() |
|
Hii ni mara
ya kwanza Juventus wanaruhusu kufungwa mabao 3 nyumbani tangu mwaka 2009
walipofungwa bao 4-1 na Bayern Munich, Juventus walimaliza wakiwa pungufu baada
ya Paulo Dyabala kuoneshwa kadi nyekundu.
Kama hujui
tu ni kwamba bao la kwanza la Madrid ndio bao la mapema zaidi kwa Cristiano
Ronaldo kuwahi kufunga katika Champions League, huku sasa Mreno huyo akiwa na
mabao 38 katika msimu huu(michuano yote) ikiwa ni idadi kubwa kuliko mchezaji
yeyote barani Ulaya.
|

![]() |
|
Sevilla nao
almanusra waishangaze Bayern Munich baada ya kupata bao la kuongoza dakika ya
32 kupitia Paulo Sarbia bao linalowafanya Munich kuwa wameruhusu bao katika
michezo yao 13 ya ugenini katika Champions League.
Lakini
Bayern walisawazisha baada ya Jesus Navas kujifunga dakika ya 37 kabla ya
Thiago Alcantara kuwahakikishia Bayern Munich uhakika wa alama tatu muhimu
katika ardhi ya ugenini.
Ushindi wa
leo unamfanya kocha wa Bayern Munich Jupp Henyckes kuwa kocha wa kwanza katika
historia kuwahi kushinda michezo 12 mfululizo katika michuano ya Champions
League.
|








No comments:
Post a Comment