Ligi Daraja la 3 Kagera:Majengo FC yaichapa 6-1 Ngara Boys huku Nzaza Stars kwa mbinde ikiifunga Ngara Stars 1-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 10, 2017

Ligi Daraja la 3 Kagera:Majengo FC yaichapa 6-1 Ngara Boys huku Nzaza Stars kwa mbinde ikiifunga Ngara Stars 1-0.

Kikosi cha  Nzaza Stars wakiomba dua mara baada ya kumaliza Mchezo wake kwenye uwanja wa Kayanga Karagwe/Kagera Jana January 09,2017.

Nzaza FC imefanikiwa kuifunga kwa mbinde goli 1-0 timu Ngara Stars zote kutoka wilayani Ngara mkoani Kagera katika mwendelezo wa Ligi soka Taifa Daraja la 3 mkoani Kagera hapo Jana January 09,2017, kwenye mchezo wa pili wa timu hizo za Kundi A katika Uwanja wa Kayanga/Karagwe na Kaitaba/Mjini Bukoba.

Goli la Nzaza FC lilifungwa na Mchezaji John dakika ya 51 ya mchezo huo huku mchezo wa saa 8 mchana wa kundi hilo, Polisi Kagera toka Manispaa Bukoba waliifunga 2-0 timu ya Nyaishozi FC ya Karagwe.
Katika Kituo cha Kaitaba/Bukoba-Michuano hiyo ya  Ligi ngazi ya Mkoa wa Kagera -Timu ya  Polisi  Jamii ya Bukoba  ilicheza na Polisi Karagwe  zote za Kundi A na Polisi Jamii kuibuka  kidedea kwa kuichapa   bao 2 -1.

Mchezo  wa jioni saa 10-Timu ya Ngara Boys kutoka Ngara ilikubali kipigo cha magoli 6-1 kutoka kwa Timu ya Majengo FC ya Manispaa Bukoba.

Kwa ushindi huo sasa Majengo FC wanafikisha pointi 6 huku Ngara Boys wakipoteza mechi ya pili mfululizo katika Ligi hiyo inayoshirikisha timu 19 toka mkoani Kagera.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad