RC Kagera alivyo Wamwagia Waratibu wa Elimu Ngara Neema ya Pikipiki. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, September 11, 2018

RC Kagera alivyo Wamwagia Waratibu wa Elimu Ngara Neema ya Pikipiki.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Bw.Marco Gaguti akiwasha moja ya Pikipiki wakati wa hafla ya makabidhiano ya pikipiki 22 kwa Waratibu wa Elimu ngazi ya Kata wilayani Ngara, iliyofanyika katika Viwanja vya Ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Ngara September 08,2018.
Maafisa Elimu Kata 22 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera wametakiwa kutumia pikipiki walizopata kuinua kiwango cha elimu katika kata zao, ili wilaya ipande kielimu na kufikia nafasi ya kwanza kimkoa na hata kitaifa.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameyasema hayo Septemba 08, 2018 katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ngara alipokuwa akiwakabidhi pikipiki 22 kwa Waratibu wa Elimu katika Kata 22 za Halmashauri hiyo.

Amewambia Maafisa Elimu hao kuwa yeye kama Mkuu wa Mkoa anapowakabidhi pikipiki hizo anatarajia kuona ubora wa elimu katika mkoa wa Kagera unaongezeka; na kuogeza kwamba kuanzia mwaka 2019 mkoa utachukua nafasi ya kwanza katika kufaulu mitihani ya darasa la saba kitaifa.

 “Tumepewa vifaa hivi tuvitunze vifanye kazi leo, vifanye kazi kesho na siku zote zijazo, ili elimu iendelee kuwa bora siyo katika mkoa wa Kagera tu, bali katika taifa zima.” Alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa wa Kagera.

Aidha Serikali imewakabidhi pikipiki 2,894 Waratibu wa Elimu katika Kata za nchi nzima kwa ajili ya kuboresha sekta hiyo na zina thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni  8 ukiwa na  malengo ya kutembelea na kukagua shule zilizopo mbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad