Mshambuliaji
wa Real Madrid na Ureno Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa
dunia wa FIFA.
|
Akizungumza
baada ya kushinda tuzo hiyo mjini Zurich, Ronaldo alisema: "Kama
nilivyowahi kusema mara nyingi, mwaka jana ulikuwa mwaka wa ndoto. Real Madrid
ilishinda Ligi ya Mabingwa, na Ureno ubingwa wa Ulaya. Ninajivunia na nina
furaha sana, na ninawashukuru wachezaji wenzangu kwa mwaka mzuri,"alisema.
|
Ronaldo, 31,
amewapiku Lionel Messi wa Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid
katika sherehe zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi.
Ronaldo pia
alishinda tuzo ya Ballon d'Or mwezi Disemba mwaka jana 2016, kufuatia mafanikio
yake katika Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Real Madrid, na pia kushinda Euro 2016
akiwa na timu ya Taifa ya Ureno.
|
Ronaldo kwa
mara ya kwanza aliibuka na mpenzi wake mpya, Georgina Rodriguez baada ya tetesi
za kwamba wapo kwenye mahusiano.
|
Ronaldo
aliisaidia Real Madrid kubeba Ubingwa wa Ulaya lakini akaisaidia Ureno Picha chini kubeba
ubingwa wa Ulaya kwenye EURO 2016 nchini Ufaransa.
|
Kwa upande
wa Kinamama, Mchezaji Bora ni Carli Lloyd wa USA.
Kocha Bora
Duniani kwa Wanaume ni Claudio Ranieri baada ya kuiwezesha Leicester City, bila
kutegemewa, kutwaa Ubingwa wa England kwa mara ya kwanza katika Historia yao.
Nae Mohd
Faiz Subri wa Penang, Malaysia ndie alitwaa Tuzo ya Puskas ya Goli Bora la
Mwaka.
Kwenye Tuzo
ya Mashabiki, Mashabiki wa Timu za Liverpool na Borussia Dortmund, kwa pamoja,
wameshinda Tuzo hii kwa tukio la kuimba wote ‘Wimbo wa Taifa wa Liverpool’
-'You'll Never Walk Alone'- Uwanjani Anfield kabla ya Mechi yao ya Robo Fainali
ya UEFA EUROPA LIGI Msimu uliopita.
|
FIFA TUZO ZA UBORA – WAGOMBEA NA MSHINDI.
MCHEZAJI BORA WANAUME:
-Wagombea: Cristiano
Ronaldo, Antoine Griezmann, Lionel Messi
-Mshindi: Cristiano Ronaldo
MCHEZAJI BORA WANAWAKE:
-Wagombea: Melanie
Behringer, Carli Lloyd, Marta
-Mshindi: Carli Lloyd wa USA.
KOCHA BORA WANAUME:
-Wagombea: Claudio
Ranieri, Fernando Santos, Zinedine Zidane
-Mshindi: Claudio Ranieri wa Mabingwa wa England Leicester
City
KOCHA BORA WANAWAKE:
-Wagombea: Jill
Ellis, Silvia Neid, Pia Sundhage
-Mshindi: Silvia Neid [Germany]
GOLI BORA [Tuzo ya Puskas]:
-Wagombea: Marlone,
Daniuska Rodriguez, Mohd Faiz Subri
-Mshindi: Mohd Faiz Subri wa Penang,
Malaysia.
**Tuzo hii inatokana na Kura za Mashabiki Duniani kote.
TUZO TOKA KWA MASHABIKI:
-Wagombea: Mashabiki
wa Den Haag, Borussia Dortmund & Liverpool na Iceland.
-Mshindi: Mashabiki wa Borussia Dortmund & Liverpool
TUZO YA UCHEZAJI WA HAKI
-Mshindi: Atletico Nacional ya Colombia
FIFA FIFPro World11 2016 – Kikosi Bora cha Mwaka 2016:
-Kipa: Neur
-Mabeki: Alves,
Pique, Ramos, Marcelo
-Viungo: Modric,
Kroos, Iniesta
-Mafowadi: Suarez,
Ronaldo, Messi
++++++++++++++++++++++++++
KURA KUPATA WASHINDI:
-Washindi wa Tuzo hizi watapatikana kwa Kura:
-Asilimia 50 ni ile ya Makepteni na Makocha wa Timu za Taifa
za Nchi Wanachama FIFA
-Asilimia 25 ya Kura itatoka kwa Kura za Mtandaoni za
Mashabiki
-Asilimia 25 ni Kura za Wawakilishi 200 wa Wanahabari kutoka
Mabara yote 6 Duniani.
|
No comments:
Post a Comment