Mhe.Alex Gashaza.
Katika
mkutano huo wananchi wamepinga hoja ya Mbunge
kwamba, haukufuatwa utaratibu wa kugawa ardhi ya kijiji hicho kwa wawekezaji
kutoka Korea Kusini.
Wamesema
kwamba wanaridhia
wawekezaji wa taifa hilo kuanzisha miradi ya maendeleo wajipatie ajira
kujikwamua kiuchumi huku wakidai ardhi iliyopo ni maeneo ya wazi hawanufaiki
nayo ukiachilia malisho ya mifugo.
|
Mmoja
wa wananchi wa kijiji hicho Mathayo
Daniel amesema ardhi hiyo imejaa ng’ombe wanaotoka kwa wafugaji wa
nje ya kijiji hicho wakiwemo raia wa nchi jirani lakini wananchi hawanufaiki
ispokuwa viongozi hivyo ardhi wawekezaji waruhusiwe kuanzisha miradi yao.
“Sisi wananchi wa kijii cha Kazingati tuliitwa na
Mwenyekiti wa kijiji, akatuuliza kuhusu kugawa ardhi tulimkubalia na
kuhitaji kupata ajira na lakini pia ardhi iliyopo katika kijiji hiki inatosha
kuwekeza unapinga wawekezaji lini tutapata ajira na kufaidika?”
Alihoji Daniel.
Naye
Johanseni Rumuli amewatuhumu
viongozi kugawa ardhi bila wananchi kushirikishwa na hivi sasa baadhi ya maeneo
ya wakulima na wafugaji yamewekewa alama za watu ambao wanatumia ardhi hiyo
bila kuridhiwa na mkutano mkuu wa kijiji na serikali ya wilaya hiyo.
|
Askari Polisi wakiimalisha Usalama eneo la Mkutano.
Mbunge
wa Ngara Mhe.Alex Gashaza
anapinga kutolewa ardhi kwa wawekezaji wa Korea Kusini baada ya kusainiwa
mkataba (MOU) wa kuchukua ardhi ekari 12,000 wa kati wananchi hawakuridhia
katika mkutano wa hadhara na ardhi ya kijiji hicho ukubwa wake ni ekari
8,000.
Aidha
madai ya Mbunge huyo ni kwamba hakuna kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri
ya wilaya ya Ngara kilifanyika kupitisha kugawa ardhi ya kijiji cha
Kazingati ambayo ilibainishwa kwenye vitongoji vya vya Muko na Msalasi
vyenye ukubwa usiozidi ekari 4,140.
"Mkurugenzi wa halmashauri aliomba ekari 1000 katika kijiji
hicho lakini mkataba wa wakezaji wamesaini ekari 12,000 kitu kinachoashiria
ukiukaji wa taratibu kwa sheria ya ardhi namba tano ya mwaka 1999"
Amesema Gashaza.
|
Ramani ya Eneo la Uwekezaji kijiji cha Kazingati,Ngara mkoni Kagera.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Ngara,Mhe. Erick
Nkilamachumu amesema, utaratibu wa kitoa ardhi ulifuatwa na malengo ni
wananchi kupata miradi kujiongeea mapato kiuchumi.
Amesema
matarajio ya halmashauri ilikuwa kupata waeekezaji kuunga mkono juhudi za
serikali za tanzania kuwa na uchumi wa kati na viwanda ambapo hata wilaya ya
ngara ingesonga mbele katika kukusanya mapato.
"Mgogoro huo hadi halmashauri iufikishe wizara ya ardhi
kwa waziri mwenye mamlaka ndiye atakayeweza kuutolea ufafanuzi badala ya
kujibia hoja mkanganyiko sijichonganishi na wananchi ".Amesema Nkilamachumu.
Mgogoro
huo wa ardhi ya kijiji hicho umesababisha mgawanyiko wa wananchi na viongozi wa
kisiasa baina yao na Mbunge huyo Alex Gashaza, pia kuwepo dalili za ukabila baina ya Wahangaza
wa Bugufi anakotoka Mbunge huyo na kabila la washubi ilipo ardhi ya hao
wawekezaji.
|
Udah punya Asuransi belum? Pasti belum, iya kan. Yuk baca artikel berikut Asuransi Kendaraan MSIG, Berkendara Tanpa Cemas kali aja setelah baca artikel berikut langsung kepincut beli asuransi. Asuransi itu penting loh.
ReplyDelete