Katika hatua
za awali Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeanza mikakati
mbalimbali ya uboreshaji wa Mapori hayo ili kuyapandisha hadhi na kuwa Hifadhi
za Taifa Tanzania.
Kwanza TANAPA imewaleta Watumishi 16 Mkoani Kagera ili
kurahisisha mchakato wa upandishwaji hadhi wa Mapori hayo na kuongeza doria kwa
kishirikiana na watumishi waliokuwepo wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania TAWA.
Watumishi
hao 16 wa TANAPA wanaongozwa na Bw. Damian Salu ambaye ni Mkuu wa Hifadhi na
Mratibu wa mchakato wa upandishwaji hadhi wa Mapori ya Akiba matano Mkoani
Kagera ambapo akiongea na Mkuu wa Mkoa Gaguti katika Pori la Burigi alisema
kuwa pamoja na TANAPA kuwa na watumishi hao 16 lakini imeanza kuchukua
mbalimbali hatua za kuboresha mapori hayo.
Bw. Salu
alisema kuwa tayari TANAPA imeanza kutengeneza miundombinu ya barabara na
tayari Kilometa 35 za barabara zimerekebishwa ili kuweka urahisi wa Watalii
wa nje na ndani kupita katika Hifadhi hizo kwa urahisi wakati wa kutalii. Pili
ni kuongeza doria katika mapori hayo ili kukomesha ujangiri katika Hifadhi za
Taifa tarajiwa.
Mikakati
mingine ni kuelimisha wananchi wanaozunguka Hifadhi tarajiwa juu ya umuhimu wa
kutunza Hifadhi na jinsi ya wao watakavyonufaika na Hifadhi hizo katika masuala
ya maendeleo ya jamii pamoja na ulinzi shirikishi kati yao na Shirika la Hidhi
za Taifa Tanzania.
Aidha, TANAPA wanaendelea na mikakati ya kuzitangaza Hifadhi
mpya zilizoko Mkoani Kagera ili wawekezaji wa ndani nje kuja kuwekeza Kagera.
Bw. Salu pia
alisema kuwa TANAPA wanao mpango wa kupandikiza aina mbalimbali nyingine za
wanyama katika Hifadhi tarajiwa ili kuongeza vivutio ambavyo ni muhimu kwa
Watalii wa ndani na nje kuja katika Hifadhi hizo kuona.
|
Fursa za Nchi Tatu Katika Pori la Ibanda.
Katika Pori
la Akiba la Ibanda Wilayani Kyerwa kuna eneo ambalo ni mipaka ya nchi tatu za
Afrika Mashariki ambapo kwa upande wa Tanzania eneo hilo la pori la akiba
linajulikana kama Kagaga, Nchi ya Uganda eneo hilo linaitwa Sophia au “Mirama
Hill” na Upande wa Rwanda panaitwa Kajitumba.
Eneo hili linatenganishwa na
Mto Kagera na Mtalii anapata fursa ya kuona mipaka ya nchi tatu kwa wakati
mmoja.
Mara baada
ya kutembelea eneo hilo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Gaguti alitoa wito kwa
wawekezaji kuona fursa hiyo ikiwa ni pamoja na Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) kujenga Hoteli na vituo vya Utalii ili kutoa fursa kwa Watalii kutoka
nchi za Rwanda na Uganda kuingia katika Hifadhi ya Taifa tarajiwa ya Ibanda
kupitia mipaka hiyo kwa kuvuka mto Kagera na kuingia katika Hifadhi bila kupita
Mipaka ya Mulongo na Rusumo.
“Hapa
tukipata wawekezaji tunatakiwa kujenga Hoteli za kisasa, vituo vya utalii ili
kama mtalii anataka kutoka Uganda au Rwanda kuja katika Hifadhi ya Taifa ya
Ibanda apite hapa na hakuna ulazima wa kupita Mulongo au Rusumo, hii ni fursa
kubwa sana lazima tuitangaze kwa nguvu zote ili tutumie nafasi ya uwepo wa
mipaka hii mitatu kupata watalii ambapo tunaweza kujenga vivuko au kupata boti
za kitalii za kuwavusa katika Mto huu wa Kagera. Alisistiza Mkuu wa Mkoa
Gaguti.
|
Wito kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera .
Wito
unatolewa kwa vijana Mkoani Kagera kuanza kuchangamkia fursa kwa kuanza kujiandaa
katika masomo ya utalii ambapo watapata ajira za kuongoz Watalii, kujiandaa
kusomea uhotelia ili kufanya kazi katika Hoteli za Kitalii zitakazojengwa
katika Hifadhi hizo za Taifa Mkoani Kagera, hayo ni pamoja na kusomea lugha
mbalimbali ili kupata fursa nzuri ya kuongoza Watalii kutoka nchi
mbalimbali na kuelezea vizuri juu ya maliasili katika hifadhi hizo.
Wawekezaji
mbalimbali hasa kwa Mkoa wa Kagera wanatakiwa kuchangamkia fursa hii ya utalii
kwa kujenga Hoteli nzuri, hususani katika Halmashauri zetu za Wilaya
zinazozunguka Hifadhi hizo tarajiwa za Taifa lakini pia Hoteli hizo kujengwa
ndani ya Hifadhi hizo pamoja na vivutio na vituo mbalimbali vya kitalii
ili kuvuti watalii wa ndani na nje ya mkoa kwa ujumla.
Utamaduni.
Wananchi
wanaozunguka katika Hifadhi tarajiwa za Taifa wanakumbushwa kujiandaa kuanzia
sasa hasa katika kutengeneza vitu malimbali vya kitamaduni ambavyo vinaweza
kuuzwa kwa watalii hasa watakaokuwa wanatoka nchi za nje ili wananchi hawa
wajipatie kipato tena kwa fedha za kigeni kupitia vivutio vya kitamaduni
vitakavyokuwa vinapatikana katika hifadhi hizo.
|
Vyakula vya Kitamaduni.
Wananchi pia wanatakiwa kuanza sasa
kulima kwa wingi vyakula vya kitamaduni kulingana na utamaduni wao na kujiandaa
kwa ajili ya kupata soko la vayakula hivyo vinavyopendelewa sana na Watalii na
kuona ni namna gani vyakula hivyo vinapikwaje au vinaandaliwaje kitamaduni na
ikumbukwe kuwa hiyo ni mmojawapo ya utalii.
Hoteli kubwa
zitahitaji vyakula hivyo kwa wingi kwa maana hiyo wakulima Mkoani Kagera hasa
ambako kila zao linakubalika vizuri kulimwa na kustawi wanatakiwa kuiona fursa
hiyo mapema ili masoko ya mazao hayo yasije kutekwa na wakulina na
wafanyabiashara kutoka mikoa jirani au pengine nchi jirani wakati fursa hiyo
ingeweza kuchukuliwa na wananchi wa Mkoa wa Kagera.
Changamoto.
Chanagamoto
kubwa ambayo bado hasa inaikumba Hifadhi ya taifa Tarajiwa ya Ibanda Wilayani
Kyerwa ni pamoja na nchi jirani zinazopakana na hifadhi hiyo kujenga Kambi ya
Wakimbizi ambayo ipo karibu sana na hifadhi hiyo jambo ambalo linapelekea
wakimbizi hao kuvuka mto Kagera na kufuata mahitaji muhimu upande wa pili kama
kuni na kuua wanyama pori kwa ajili ya kupata kitoweo au chakula.
Pia nchi
jirani zinazopakana na Hifadhi za taifa tarajiwa Mkoani Kagera zimeruhusu
makazi ya wananchi kupakana na hifadhi hizo jambo ambalo linachochea ujangiri
katika hifadhi pale wananchi wa nchi hizo wanapovuka na kutaka kuendesha
shughuli za uwindaji kwenye hifadhi.
Mwisho bado
wananchi hasa katika Mkoa wetu wa Kagera hawajachangamkia fursa ya kuwekeza
katika Hifadhi hizo na kutoa nafasi kwa wawekezaji kutoka nje ambapo hapo
baadae wananchi hawa wa kagera wanaweza kuanzisha migogoro kwa kutokuona
manufaa ya hifadhi za taifa tarajiwa kwao.
Ni muhimu sana wananchi wazawa
kuanza kuchangamkia fursa hizi mara moja ili kujiongezea kipato. Karibu TANAPA
Kagera, Karibu Tutalii Kagera.
|
No comments:
Post a Comment