MAPINDUZI CUP 2016:- Yanga SC na Azam FC sare leo January 06,2016 ni Simba SC na URA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, January 06, 2016

MAPINDUZI CUP 2016:- Yanga SC na Azam FC sare leo January 06,2016 ni Simba SC na URA.

Wachezaji wa Azam na Yanga wakiwa katika zogo lililosababishwa na Ngoms ns Pascal Wawa
Wachezaji wa Azam na Yanga wakiwa katika zogo lililosababishwa na Ngoma na Pascal Wawa wakati wa mchezo wao wa Mapinduzi Cup 2016,Jana usiku January 05.

Jana,January 05, 2016 usiku lilipigwa pambano kati ya Yanga SC dhidi ya Azam FC mchezo wa Mapinduzi Cup 2016 ambao ulikuwa umejaa ubabe mwingi ambapo limemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1 huku mchezo huo ukitawaliwa na  mpira wa kibabe na timu hizo kushindwa kuonesha burudani kwa mashabiki waliofururika kushuhudia mchezo huo.

Kipre Tchetche alianza kuifungia Azam FC bao la kuongoza lakini bao hilo halikudumu kwa dakika 90 kwani Vincent Bosou alisawazisha bao kwa upande wa Yanga SC ambalo nalo lilizua utata huku wachezaji wa Azam FC wakipinga maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo kulikubali goli hilo.

Wawa (kulia) akijibizana mbovu na Donald Ngoma
Wawa (kulia) akijibizana mbovu na Donald Ngoma aliyeshikiliwa na golikipa wa Azam Aishi Manula

Kutokana na nidhamu mbovu iliyooneshwa na wachezaji wa timu zote mbili pamoja na viongozi wao wakiwemo makocha, mwamuzi wa mchezo huo alilazimika kutoa kadi nyingi za njano pamoja na kadi moja nyekundu ambayo ilikwenda kwa John Bocco.
Aishi Manula akijitahidi kumshawishi Donald Ngoma apunguze vurugu
Aishi Manula akijitahidi kumshawishi Donald Ngoma apunguze vurugu

Kiukweli mashabiki wa soka wa Zanzibar walijitahidi kujitokeza uwanjani kushuhudia mchezo huo lakini hakukuwa na jipya zaidi ya wacheaji kupigana viatu hadi ngumi pia.
Mashabiki walifurika uwanjani hadi wakakaa chini kufuatia kukosa nafasi
Mashabiki walifurika uwanjani hadi wakakaa chini kufuatia kukosa nafasi

Mechi hiyo ilimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1 Azam FC na Yanga SC zinakimbizana kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Azam FC wako kileleni wakati Yanga SC wao wako nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi mbili.
Mashabiki wa Yanga wakiisapport timu yao
Mashabiki wa Yanga SC wakiisapport timu yao

Matokeo ya jana, January 05,2016 yanaiweka pabaya Azam FC ambayo imetoka sare kwenye michezo miwili hivyo inapointi mbili wakati Yanga SC  na Mtibwa Sugar zikiwa na pointi nne kila moja lakini zikitofautishwa kwa tofauti ya wastani wa magoli ya kufungwa na kufunga.
????????????????????????????????????
Mechi ilianza vizuri lakini kadiri muda ulivyokwenda ndivyo mambo yalivyochacha
Mechi ilianza vizuri lakini kadiri muda ulivyokwenda ndivyo mambo yalivyochacha
Kikosi cha Azam FC kilichoanzishwa na koch Stewart Hall dhidi ya Yanga
Kikosi cha Azam FC kilichoanzishwa na koch Stewart Hall dhidi ya Yanga SC
Watoto nwa Jangwani walianza kwenye mchezo dhidi ya Azam FC
Kikosi cha  Jangwani ,Yanga SC kilichoanza kwenye mchezo dhidi ya Azam FC...Picha kwa Hisani ya Shaffi Dauda.

Jumatano Januari 6,2016

1615 Jamhuri v JKU

2015 URA v Simba SC
 


Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad