MAPINDUZI CUP 2016:- Mtibwa Sugar hao na Matumaini dhidi ya Mafunzo wakiichapa 1 - 0. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Tuesday, January 05, 2016

demo-image

MAPINDUZI CUP 2016:- Mtibwa Sugar hao na Matumaini dhidi ya Mafunzo wakiichapa 1 - 0.

.com/simgad/
.com/blogger_img_proxy/

Timu ya Mtibwa Sugar imeisukuma nje ya mashindano timu ya Mafunzo ya visiwani Zanzibar baada ya kuifunga kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa leo Jumanne January 5, 2016 kwenye uwanja wa Amaan.

Said Bahanuzi ndiye aliyeitupa nje Mafunzo kwani goli lake la dakika ya 12 kipindi cha kwanza lilidumu mpaka dakika zote 90 za mchezo zinamalizika.
.com/blogger_img_proxy/

Ushindi huo unaipa matumaini Mtibwa Sugar kwa sababu imefikisha pointi 4 baada ya michezo miwili.

Matokeo ya leo,Jumanne January 05,2016 ni faraja kwa Mtibwa ambao goli lao la ushindi kwenye mchezo dhidi ya Azam FC lilikataliwa na mwamuzi wa pembeni Dalila Jaffar Mtwana ambaye tayari ameshawajibishwa kwa kuondolewa kwenye orodha ya waamuzi wanaoendelea kuchezesha mashindano hayo.
.com/blogger_img_proxy/

Matokeo hayo yanaiondoa kwenye mashindano timu ya Mafunzo ambayo imepoteza michezo yake miwili na kubakiza mchezo mmoja ambao utakuwa ni wa kukamilisha ratiba itakapocheza dhidi ya Azam FC.


Jumapili Januari 3,2016


Yanga 3 – 0 Mafunzo 

Mtibwa Sugar 1 – 1 Azam FC 

Jumatatu Januari 4,2016

JKU 1 - 3  URA 

Simba 2 – 2 Jamhuri 

Jumanne Januari 5,2016

Mafunzo 0 – 1  Mtibwa Sugar

2015 Azam FC v Yanga

Jumatano Januari 6,2016

1615 Jamhuri v JKU

2015 URA v Simba
.com/blogger_img_proxy/
Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *