Hii ndo orodha ya nchi zilizochukua medali katika michuano ya OLIMPIKI 2012 LONDON kwa sasa. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Monday, August 06, 2012

demo-image

Hii ndo orodha ya nchi zilizochukua medali katika michuano ya OLIMPIKI 2012 LONDON kwa sasa.

.com/simgad/
1

Aidha kwenye  Uwanja wa Millenium Stadium huko Cardiff, Wenyeji wa Mashindano ya OLIMPIKI LONDON 2012 Team Britain walitolewa nje baada ya Daniel Sturridge kukosa penati katika Tombola ya Mikwaju Mitano ya Penati waliposhindwa kwa penati 5-4 baada ya kutoka sare bao 1-1 na Korea ya Kusini katika Dakika 90 na nyongeza ya Dakika 30 kutozaa Mshindi huku pia wakikosa penati ndani ya Dakika 90 iliyopigwa na Aaron Ramsey.


Korea ya Kusini wanaungana na Mexico, Japan na Brazil kwenye Nusu Fainali zitakazochezwa Jumanne Agosti 7.

  

Korea ya Kusini walitangulia kufunga kwa bao la Ji katika Daika ya 29 lakini Team Britain walirudisha baada ya Aaron Ramsey kufunga kwa penati katika Dakika ya 36 lakini alikosa penati nyingine Dakika 3 tu baadae baada ya Kipa kuicheza.

 

Hadi mapumziko bao zilikuwa 1-1 ambazozilidumu hadi mwisho wa Dakika 120. 

2
Katika Mechi ya kwanza Japan ilifanikiwa kuichakaza Egypt kwa bao 3-0 na Egypt ilicheza Mechi hiyo kuanzia Dakika ya 41, ikiwa bao 1-0 nyuma, Mtu 10 kufuatia Saad Samir kupewa Kadi Nyekundu.


Bao za Japan zilifungwa na Kensuke Nagai, Dakika ya 14, Maya Yoshida, Dakika ya 79 na Yuko Otsu, Dakika ya 83.


Mechi ilyofuatia, Mexico waliwachapa Senegal bao 4-2 katika Dakika 120 za mchezo baada ya kutoka bao 2-2 katika Dakika 90.



Mechi ya 3 ya Robo Fainali ilikuwa kati ya Brazil na Honduras na Brazil kuibuka kidedea kwa ushindi wa bao 3-2 lakini walikuwa ni Honduras ambao mara mbili walitangulia kufunga kwa kuanza na bao la Dakika ya 12 lililofungwa na Martinez.

3
MATOKEO:
ROBO FAINALI
Jumamosi Agosti 4

Japan 3 Egypt 0
Mexico 2 Senegal 2 [Dakika 120: 4-2]
Brazil 3 Honduras 2
Team GB 1 Korea Kusini 1 2 [Dakika 120: 1-1, Penati 4-5]

NUSU FAINALI
Jumanne Agosti 7

Mexico v Japan, Wembley (Saa 1 Usikui)
Korea Kusini v Brazil (Saa 3 Dak 45 Usiku)

mo

Mohamed Farah wa Great Britain akishangilia baada ya kushinda medali ya dhahabu kwenye mbio za wanaume mita 10,000 katika mashindano ya Olimpiki 2012 kwenye uwanja wa Olympic,  jijini London.


1327790_M01

Gold medalist Tiki Gelana of Ethiopia rests at the finish line on The Mall after the Women's Marathon on Day 9 of the London 2012 Olympic Games.


1327778_M01
Katika  Mechi 4 za Wanawake za Robo Fainali na matokeo yake ni kuwa Wenyeji Britain wametupwa nje pamoja na Timu inayocheza ‘Soka Tamu’ Brazil.


Timu zilizoshinda na kutinga Nusu Fainali ni Mabingwa wa Dunia Japan, Mabingwa watetezi wa Olimpiki USA pamoja na Ufaransa  na Canada.


MATOKEO:
ROBO FAINALI
Ijumaa Agosti 3

Sweden 1 France 2
USA 2 New Zealand 0
Brazil 0 Japan 2
Britain 0 Canada 2


MARTA
Mechi zao za Nusu Fainali zitachezwa Jumatatu Agosti 6.

NUSU FAINALI
Jumatatu Agosti 6

France v Japan, Wembley (Saa 1 Usikui)
Canada v USA, Manchester (Saa 3 Dak 45 Usiku)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *