![]() |
Aidha Serikali
ya Tanzania imetoa pikipiki hizi kwa Maafisa Elim Kata, ili waweze kusimamia
ubora wa elimu kupitia mpango wa kukuza stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu
KKK na kufika kila kata kwa wakati ili kuinua kiwango cha elimu.
“Kama zilivyo Halmashauri nyingine hapa nchini ambazo zilikuwa
na tatizo la watoto wa shule za msigni kushindwa kusoma, kuandika na kuhesabu,
Halmashauri ya Ngara nayo bado inachangamoto hiyo, lakini naamini pikipiki hizi
zitakuwa msaada mkubwa katika kutokomeza tatizo hili.” Alisema
Mkurugenzi huyo Mtendaji Bw. Bahama.
Pikipiki
hizo ni mkakati wa Serikali katika kutekeleza sera ya elimu ya mwaka 2014,
inayomtaka mtoto wa kitanzania amalizapo elimu ya msigi awe na maarifa, mahiri,
na uwezo wa kuleta maendeleo yake binafsi na ya taifa.
Bw.Bahama ametoa rai kwa maafisa hao
kuhakikisha wanavitunza na kwamba Serikali inatendelea kuboresha sekta ya elimu
ili kuzalisha wataalamu watakaotumiwa kwenye uchumi wa viwanda.
Akifafanua
jinsi usafiri huo utakavyowasaidia katika utendaji kazi wao,mmoja wa Afisa Elimu
Kata ambaye jina lake limehifadhiwa, amesema pamoja na kufuatilia suala la KKK,
bado atakuwa na nafasi ya kufuatilia masuala ya elimu, aliyoyataja kuwa ni
maandalio ya masomo, mahudhurio ya wanafunzi na utendajikazi wa walimu katika
shule za msingi na za sekondari katika kata zao.
|
Post Top Ad
Tuesday, September 11, 2018

Serikali yakabidhi Pikipiki 22 Maafisa Elimu Ngara Kusimamia Ubora wa Elimu.
Tags
# HABARI
# MATUKIO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
Makala Inayofuata
RC Kagera alivyo Wamwagia Waratibu wa Elimu Ngara Neema ya Pikipiki.
Makala Iliyopita
Rais Dkt. John Magufuli Ametimiza Ahadi kwa JWTZ Kuhusu Ufugaji wa Samaki Mkoani Mara.
Muonekano wa Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
AnonymousDec 10, 2019Viongozi Wilayani Kasulu watakiwa Kuimarisha Usalama Katika Korongo la Bolelo.
AnonymousJun 29, 2019Shirika la Ndege la Tanzania Laanza Safari za Afrika Kusini Leo 28/06/2019.
AnonymousJun 28, 2019
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment