![]() |
|
Wakimbizi
hao waliofariki dunia na kuzikwa ni Tyisenge Minani, Nyabenda Leonia,
Nyandwi Veronica, Miburo Gervas, Barutwanayo Salvatory na Buchumi Casmir na
Shughuli hiyo ya mazishi imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na
Mashirika yanayohudumia Wakimbizi akiwemo Mwakilishi wa Shirika la UNHCR hapa
nchini Tanzania, Bi. Chansa Kapaya. Katika ajali hiyo Pia walifariki Watanzania wawili ambao ni Osilia Mabuye aliyekuwa Mfanyakazi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM na Mkazi wa Kijiji cha Kasharazi aliyepamiwa na basi lililopoteza mwelekeo baada ya kufeli mfumo wa breki na kusababisha ajali. |
![]() |
|
Mkuu wa mkoa
wa Kigoma, Brigedia General Mstaafu Emmanuel Maganga wakati wa mazishi
hayo,amewataka wakimbizi raia wa Burundi waishio kwenye makambi hapa nchini
kutokatishwa tamaa na mtu yeyote katika kuhiyari kurejea nchini Burundi kwani
kwa sasa kuna amani ya kutosha.
|

![]() |
|
Aidha mpaka sasa Majeruhi waliokuwa wamelazwa
katika Hospitali ya Nyamiaga wote wameruhusiwa baada ya afya zao kuimarika na
wamesafirishwa kurejea makwao nchini Burundi wakati katika Hospitali ya
Murugwanza wakibaki majeruhi watatu (zote za wilayani Ngara mkoani Kagera )
huku waliopata rufaa kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza wapo
Wakimbizi Majeruhi 25.
Habari Na radiokwizera.co.tz
|









No comments:
Post a Comment