Wadau waitaka TANROADS Kujitafakari Upya Kuhusu Ubovu wa Barabara Nchini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 06, 2018

Wadau waitaka TANROADS Kujitafakari Upya Kuhusu Ubovu wa Barabara Nchini.

Muonekano wa mashimo mawili barabarani katika barabara ya Igunga –Singida linalotajwa kuwa chanzo cha ajali ya Basi la City Boy kugongana uso kwa uso na Fuso eneo la Makomero ambapo tairi la Fuso lilipasuka na kupoteza muelekeo.


TAARIFA RASMI NI HII TULIOIPATA KUTOKA KWA INSPECTOR HARDSON KAIMU RTO MKOA WA TABORA.

Gari T486 ARB FUSO ikiwa na mzigo wa viazi ikitokea singida kuelekea Igunga tairi ya kulia litumbukia KTK mashimo mawili barabarani kisha kupasua tairi na rim kupinda & mfumo wa usukani kukatika maungio ya steering rod na steering box kisha gari kukosa uelekeo na kugonga basi la abiria T983 DCE Scania kampuni ya city boy. 

Jumla ya watu 12 wamepoteza maisha , 10 eneo la tukio, 2 wakiwa wanapelekwa Hospitali ya Wilaya ya Igunga. 

Jumla ya majeruhi 46 wamefikishwa Hospitali ya wilaya ya Igunga kwa matibabu, kati yao 3 ni mahututi amapo ME 02 wamepelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza na KE 01 amepelekwa Hospitali ya Nkinga .

Dereva wa basi amekufa papo hapo. Wahusika wa FUSO kwa taarifa za awali inasemekana wamekimbia baada ya ajali hii.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameliagiza Jeshi la Polisi kuwatoza faini, kuwaweka ndani madereva wanaovunja sheria za barabarani na kusababisha ajali kizembe na wasiachiwe mpaka watakapofikishwa Mahakamani.

Mwigulu ametoa agizo hilo  Alhamisi, Aprili 5, 2018 bungeni Mjini Dodoma wakati akitoa taarifa ya ajali iliyotokea wilayani Igunga usiku wa kuamkia leo, ajali iliyohusisha lori aina ya fuso na basi la abiria la Kampuni ya City Boys na kuua watu 12 huku wengine 46 wakijeruhiwa.

Taarifa za awali tulizopewa zilieleza chanzo cha ya ajali hiyo sio mashimo ya barabarani pekee yake bali ni mwendokasi wa dereva wa fuso ambaye aliligonga basi hilo. Wengine walipita mchana kutwa kwenye hayo mashimo yeye akaja kusababisha ajali usiku. 

Naliagiza Jeshi la Polisi popote pale watakapomkamata dereva anatembea mwendokasi pamoja na hiyo ya kutoza faini, wamuweke ndani wasimuachie mpaka pale watakapompeleka Mahakamani ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa”, amesema Mwigulu.

Pamoja na hayo, Mwigulu ameendelea kwa kusema “endapo dereva huyo akitoka Mahakamani na kama rekodi zake ni mwendokasi basi anyang’anywe leseni yake ili asiweze kuendelea kuendesha magari yanayosababisha ajali na kupoteza maisha ya watu kama hivi jana ilivyotokea”.

Aidha, Rais Magufuli amewataka viongozi wote wanaohusika na usimamizi wa usalama wa barabarani kutafakari kwa nini ajali nyingi zimekuwa zikitokea katika maeneo yaleyale na kutafuta ufumbuzi ili kuepusha madhara ya watu kupoteza maisha, kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza mali.
Aidha Ujumbe wa Umoja Wa Madereva Wa Mabasi Makubwa Tanzania - Uwamata wameomba ;….Nadhani ifike kipindi sasa kila MTU awajibike kwa nafasi yake, ndugu zetu TANROAD mkoa wa TABORA haya mashimo tunayapigia sana kelele ,sitaki kuamini kwamba hayaoni na msisubiri mpaka yatokee maafa ndo mtengeneze hayo mashimo kama ilivyokua changarawe pale mafinga nayo ilikua kama hii.

Eneo hatarishi kwa mashimo ni Nyasamba, Hungumalwa, Mwanza, Nanga, Igunga road, Makomero, n.k tunawaombeni sana mzibe haya mashimo.

Fuatia tamko lako lile tu la Bungeni tayari madereva wengi usiku huu wanalala lockap kisa wemezidisha speed 82 badala ya 80 achilia mbali tumepewa ziada ya ya speed 5 na gari zina VTS.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad