|
Picha ya
pamoja ya Mabingwa Bakoba FC na Mdhamini wa Ligi hiyo ya Kamala Cup 2018 pamoja
na Mgeni rasmi na Viongozi wengine.
|
|
Mabingwa
Bakoba FC wakiwa wamebeba Mwali wao.
Ligi hii ya Kamala Cup 2018 ilianza Mwezi Februari tarehe 18, 2018 na kushirikisha Timu za Kata 16 na hii leo April 2, 2018 imehitimishwa kwa Timu ya Bakoba kuibuka Bingwa.
Mshindi wa Pili wa mashindano hayo , Ijuganyundo FC
aliondoka na Tsh Milioni 1.8 huku wa 3 Timu ya Kitendaguro FC ikiondoka na Tsh
Milioni 1.2.
|
|
Ndg. Salum
Umande Chama akiongozana na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Bukoba Bw.
Deodatus Kinawilo pamoja na mdhamini wa Ligi hii Diwani Kamala Kalumuna (kulia)
kwenda Uwanjani kukabidhi Wachezaji zawadi zao.
|
|
Mgeni rasmi
Mkuu wa Wilaya Bukoba Bw. Deodatus Kinawilo akitoa neno wakati wa ufungaji wa
Ligi hiyo ya Kamala Cup 2018.
Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo (katikati) ndiye alikuwa mgeni Rasmi katika Fainali hii iliyohitimishwa April 2, 2018 na kukitaka Chama cha Soka mkoa KRFA kwa kushirikiana na Vyama vya Soka ngazi za wilaya kuhakikisha kupitia mashindano madogo madogo yanayochezwa mkoani humo ili kuibua Timu nyingine zitakazoungana na Timu ya Kagera Sugar Ligi kuu.
Naye
muandaaji wa Mashindano hayo ya Kamala Cup 2018 , Diwani Kamala Kalumuna
amebainisha kuwa Jumala ya Tsh Milioni 11.8
kukamilika na Timu ya Bakoba Kuibuka
Kidedea kwa kuifunga Timu ya Ijuganyondo Fc Bao 3-0.
Picha zote na Faustine
Ruta, Bukoba.
|
|
Kikosi cha
Timu ya Bakoba FC kilichoifumua Ijuganyondo Fc kwenye mchezo wa fainali Kamala Cup 2018.
|
|
Kikosi cha
Timu ya Ijuganyondo Fc kilichoanza mchezo wa fainali Kamala Cup 2018.
|
|
Wachezaji wa
Timu ya Ijuganyondo wakiomba katikati ya Uwanja muda mfupi na kuanza mchezo huo
kwa kasi ambao mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika ilikuwa 0-0.
|
|
Mkuu wa
Wilaya Bukoba Bw. Deodatus Kinawilo(katikati) kulia ni Ndg. Salum Umande Chama
wakiwa meza kuu.
Ndg. Salum Umande Chama akiteta jambo na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Bukoba Bw. Deodatus Kinawilo meza kuu wakati mtanange unaendelea. |
|
Mwali wa
mshindi wa Kwanza Kamala Cup 2018.
|
|
Makombe ya
Mshindi wa Kwanza, wa Pili na Watatu Kamala Cup 2018.
|
|
Huku
Mashabiki wakimpogeza kwa Ligi hiyo ambayo ilikuwa ikishehenesha Mashabiki
kibao Uwanjani hapo Kaitaba. Pia Mdhamini huyo amesema Ligi hiyo ni Endelevu na
Mwaka kesho 2019 ataiboresha zaidi ya mwaka huu.
|
|
Taswira mbalimbali uwanjani Kaitaba ,watu waliingia kwa wingi wakati wa
Fainali Kati ya Timu ya Bakoba FC dhidi ya Ijuganyondo FC.
|
|
Kipa wa
Ijuganyondo Fc hakuona ndani....
|
|
2-0 Baadhi
ya Wachezaji wa Bakoba Fc wakipongezana kwa bao.
|
|
3-0 Ezekiel
Izack akipongezwa kwa kumwagiwa maji mara baada ya kuipachikia bao la tatu Timu
ya Bakoba FC.
|
Mashabiki mnasemaje?????





No comments:
Post a Comment