CAF yaizuia Yanga SC kutowatumia Wachezaji hawa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 04, 2018

CAF yaizuia Yanga SC kutowatumia Wachezaji hawa.

Shirkisho la soka barani Afrika CAF leo April 3 2018 kutoka makao makuu ya shirikisho hilo Cairo Misri, limetoa taarifa rasmi kwa vilabu vya Yanga SC ya Tanzania na Wolaitta Dicha SC ya Ethiopia kuwa kuna wachezaji hawatoruhusiwa kuwatumia.

CAF wametuma taarifa inayowazuia Yanga kuwatumia wachezaji wake wanne ambao ni Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Papy Tshishimbi na Said Juma huku Dicha wakikatazwa kuwatumia wachezaji wake wawili ambao ni Teklu Tafese na Eshetu Mena katika mchezo dhidi yao.
Yanga SC ya Tanzania na Wolaitta Dicha SC ya Ethiopia watacheza mchezo wao wa kwanza wa mtoano wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika jijini Dar es Salaam kati ya April 6-8,2018 hivyo wachezaji hao hawaruhusiwi kutumika kutokana na kutumikia adhabu ya kadi za njano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad