M4C yazoa makada 201 wa CCM kwa Dk. Magufuli - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, October 02, 2012

M4C yazoa makada 201 wa CCM kwa Dk. Magufuli

Mikutano ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) inayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  Mkoa wa Geita, imezoa makada 201 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwamo Mwenyekiti wa  Kitongoji cha Buhungu, Kata ya Kigongo.



 Makada waliotimkia Chadema kutoka Jimbo la Chato linalowakilishwa na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kwa nyakati tofauti, wanatoka katika Kijiji cha Muganza, Kasenga, Busaka na Igando, Kata ya Bwera, ambako chama hicho kimefanya mikutano ya hadhara.


Wana CCM hao walidai wamekihama chama hicho kwa sababu wamechoshwa na mwenendo wa siasa zake, walizodai zimechangia maisha ya wananchi kuwa magumu.



Chanzo: Nipeshe.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad