Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya gari iliyohusisha basi la abiria mali ya kampuni ya KRF na lori la mizigo katika kijiji cha Ngongwa wilayani Shinyanga, imeongeza na kufikia watu wane huku watu kumi wakifariki katika ajali mbaya eneo la Mbalizi mkoani Mbeya. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, October 02, 2012

Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya gari iliyohusisha basi la abiria mali ya kampuni ya KRF na lori la mizigo katika kijiji cha Ngongwa wilayani Shinyanga, imeongeza na kufikia watu wane huku watu kumi wakifariki katika ajali mbaya eneo la Mbalizi mkoani Mbeya.


Hili ni Basi la Dar Express kutoka Arusha kwenda Dar linateketea kwa moto eneo la Segera, mkoani Tanga, abiria wote 65 wamenusurika. Picha zote na Tanga Yetu Blog.

Aidha huko Mkoani Shinyang’a  ,idadi ya watu waliofariki katika ajali ya gari iliyohusisha basi la abiria mali ya kampuni ya KRF na lori la mizigo katika kijiji cha Ngongwa wilayani Shinyanga, imeongeza na kufikia watu wane.



Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa shinyanga Bw Onesmo Ryanga, amesema idadi ya watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo imefikia 26 hadi sasa.


Awali akithibitisha kutokea kwa ajili hiyo kaimu kamanda huyo wa polisi amesema, basi lililohusika katika ajali hiyo linafanya safari zake kati ya Dar es salaam na Bukoba.


Bw Ryanga amesema, ajali hiyo imetokea leo majira ya saa kumi na mbili asubuhi  katika eneo la barabara ya Kahama kuelekea Bukombe.



Huko mkoani Mbyea nako kumetokea ajali mbaya eneo la Mbalizi ambapo magari mawili yamegongana na kuwaka moto na kuna taarifa kuwa watu wameripotiwa kufariki dunia huku Mbunge wa wa Viti maalumu Bi.Mary Mwanjelwa akiwemo katika ajali hiyo na katibu wake akiteketea kwa moto.

 


Hivi ndivyo  picha za ajali ya mbalizi mbeya magari yakiwaka moto baada ya kugongana leo na kusababisha vifo vya watu kumi.




Pia wananchi mbalimbali pamoja na mkuu wa mkoa wa Mbeya Bw.Abbas Kandoro wanaonekana wakishuhudia ajali hiyo huku wengine wakiendelea kuokoa waliopata ajali na Askari wa jeshi la polisi wakiimarisha usalama.

Picha zote na Mbeya yetu.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad