UCHAGUZI MKUU 2015-TANZANIA:-Kura za ushindi Urais hizi hapa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, September 11, 2015

UCHAGUZI MKUU 2015-TANZANIA:-Kura za ushindi Urais hizi hapa.

Wagombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Edward Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

 Zimebaki siku 45 kuanzia leo kabla ya kufikiwa siku ya kupiga kura Oktoba 25 mwaka huu,2015 -Uchunguzi uliofanywa na Nipashe umebaini kuwa mikoa hiyo tisa, ikiwamo yenye majiji makubwa ya Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya, ndiyo yenye watu wengi zaidi waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa kutumia mfumo wa Kielektroniki (BVR). 

Takwimu zilizokusanywa na Nipashe kwa siku kadhaa kutoka katika ofisi za waratibu wa uchaguzi wa mikoa mbalimbali nchini zinaonyesha kuwa kwa ujumla, mikoa hiyo tisa ina jeuri ya kutoa rais ajaye kwani ina mtaji wa kura zinazozidi asilimia 50.

Taarifa za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) zinaonyesha kuwa hadi kufikia Julai 30, 2015 na hata baada ya kuongezwa siku nyingine nne katika wiki ya kwanza ya Agosti, 2015 ili kukamilisha kazi ya uandikishaji kwa kutumia BVR,  idadi ya Watanzania waliojiandikisha ilifikia 23,782,558, sawa na asilimia 99.5 ya matarajio.

Kati ya hao, Nipashe imebaini kuwa watu 12,119,263 wanatoka katika mikoa  tisa inayoongozwa na Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya; na ambayo kimahesabu ni sawa na asilimia 50.96 ya watu wote waliojiandikisha.  


Mbali na Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya, mikoa mingine kati ya tisa iliyo na mtaji mkubwa wa kura zinazotosha kutoa mshindi wa urais Oktoba 25 ni Tanga, Arusha, Morogoro, Tabora, Dodoma na Kagera.

Dk. Magufuli wa CCM na Lowassa wa Chadema anayewakilisha pia muungano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya NCCR-Mageuzi, NLD na Chama cha Wananchi (CUF), wanachuana pia na Fahmy Dovutwa wa UPDP, Hashim Rungwe wa Chama cha Umma (Chauma), Maximillian Lymo wa TLP, Anna Mghwira wa ACT-Wazalendo, Chief Lutasola Yemba wa ADC na Janken Kasambala wa NRA.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Ibara ya 41 (6), inaeleza kuwa mgombea yeyote wa nafasi ya urais atakayepata kura nyingi dhidi ya wagombea wengine ndiye atakayetangazwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Sheria ya Taifa ya Uchaguzi ya Mwaka 1985 (Sura ya 343), vifungu vya 35E na 35F inatoa mamlaka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumtangaza mgombea aliyepata kura nyingi kuwa mshindi wa nafasi ya urais.

Kwa sababu hiyo, mgombea yeyote atakayefanikiwa kupata asilimia 100 ya kura katika mikoa hiyo tisa atajihakikishia kuwa rais ajaye kwa ushindi wa zaidi ya asilimia 50, hata kama atapata kura za idadi ndogo katika maeneo mengine ya nchi.SOMA ZAIDI UTAFITI HUU KWA KUBOFYA HAPA.

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad