HISTORIA:-Mjue Mufti mpya wa Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, September 11, 2015

HISTORIA:-Mjue Mufti mpya wa Tanzania.

Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zuberi Bin Ally, akiwashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) baada ya kumchagua mjini Dodoma jana/September 10,2015. PICHA NA IBRAHIM.

 Hatimaye Sheikh Abubakar Zubeir ametangazwa kuwa Mufti baada ya kushinda nafasi hiyo bila mpinzani mjini hapa jana, huku akiwataka Waislamu na Watanzania wengine kuhakikisha wanalinda amani na utulivu uliopo nchini.

Katika kinyang’anyiro hicho Sheikh Zuberi, alikuwa na wenzake watatu ambaye ni Sheikh Hamis Mtupa, Sheikh Hassan Kiburwa kutoka mkoa wa Kigoma na Sheikh Ally Mkoyogole kutoka Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo mjini Dodoma jana,September 10,2015, Sheikh Zubeir aliwashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kwa kumuamini na kuahidi kulitumikia baraza hilo na Waislamu wote kwa uadilifu mkubwa.
MUFTI ZUBEIR NI NANI? 

Sheikh Zubeiri ni Mufti wa tatu wa kuchaguliwa. Anashika nafasi hiyo kumrithi Mufti Shaaban Issa Bin Simba aliyefariki Juni 22, mwaka huu 2015. 

Mufti Simba alishikia nafasi hiyo kutoka kwa Mufti wa kwanza, Sheikh Hemed Bin Juma bin Hemed aliyefariki mwaka 2002.

Mufti Zuberi  amezaliwa mwaka 1953 mkoani Tanga na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Naibu Mufti wa Tanzania na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa kwa miaka 22. Pia amewahi kuwa Naibu Kadhi Mkuu.

Kijiji alichozaliwa ni cha Kwamndolwa Old  Korogwe (Tanga). Amewahi vilevile kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Taifa Bakwata baada ya kuteuliwa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Hemed Bin Jumaa Bin Hemed. Alikuwa msaidizi wa Mufti wa kwanza, Bin Hemed tangu 1984 hadi 2002..

ELIMU

Mufti Zubeir ana Shahada ya Sheria na Uongozi wa Dini aliyoipata katika vyuo vya ndani na nje ya nchi. Awali, alisoma hadi darasa la nane mkoani Tanga. Amesoma pia katika vyuo mbalimbali vya nchi za Misri na Mombasa nchini Kenya. 

Mufti Zubeir vilevile ni Mkuu wa Chuo cha Kiislamu cha Salafia kilichopo Bunju, jijini Dar es Salaam, chenye wanafunzi 1,500 na kinachofundisha masuala ya dini kunzia ngazi ya cheti hadi shahada.

Ushiriki wake katika shughuli za kijamii ni pamoja na kuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya kitaifa ya viongozi wa dini na serikali na pia ni Makamu Mwenyekiti wa Skauti. 

Papo kwa Papo >>>> Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na mimi hapa…..FACEBOOK , TWITTER INSTAGRAM , Pia tutumie tukio la Picha kwa WhatsApp +255789925630.  


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad