![]() |
|
|
Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara, Wekundu wa msimbazi Simba
SC wameendeleza wimbi la ushindi baada
ya kuilaza mabao 2-1 timu ya Ruvu
Shooting ya Pwani, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shukrani
kwake mshambuliaji chipukizi, Christopher Edward aliyeingia kipindi cha pili
kuchukua nafasi ya Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwa kufunga bao la ushindi dakika
ya 80 na kuifanya Simba ifikishe pointi tisa baada ya kucheza mechi tatu, nyavu
zake zikitikiswa kwa mara ya kwanza leo.
Simba sasa
inaendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi saba, wakati
watani wao wa jadi, Yanga wana pointi tatu tu baada ya mechi tatu.
![]() |
|
Ruvu
Shooting; Benjamin Haule, Michael Pius, Mau Bofu, George Michael, Said Suzan,
Gideon David, Abdulrahman Mussa, Hassan Dilunga, Paul Ndauka/Seif rashid,
Hussein Said na Said Dilunga.
|
Hadi
mapumziko, Simba walikuwa tayari mbele kwa bao 1-0, lililowekwa kimiani na
mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. dakika ya 29,
akiunganisha krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’.
Katika
dakika ya 45, kipa Benjamin Haule wa Ruvu Shooting alipangua mkwaju wa penalti
wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Daniel Akuffor baada ya beki mmoja wa
timu hiyo kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Kipindi cha
pili, Ruvu Shooting inayofundishwa na kocha maarufu nchnini, Charles Boniface
Mkwasa ilisawazisha bao dakika ya 80, baada ya Seif Rashid kutumia vizuri
makosa ya beki Juma Nyosso dakika ya 75.
Seif
aliupitia mpira miguuni mwa Nyosso, ambaye alianzishiwa na kipa Juma Kaseja na
kutokana na kuchelewa kuamua, akasababisha kilichotokea.
![]() |
|
Shukrani
wake, chipukizi Edward aliyeifungia bao la ushindi Simba inayofundishwa na
Mserbia, Milovan Cirkovick dakika ya 80.
|
Ratiba ya mechi zijazo Ligi kuu soka Vodacom Tanzania bara.
Septemba
26.
Coastal Union v
Kagera Sugar[Mkwakwani, Tanga]
Polisi Morogoro v
Toto Africans [Jamhuri, Morogoro]
Septemba
28.
Azam v JKT Ruvu
[Azam Complex, Dar es Salaam]
Septemba
29.
JKT Oljoro v
Mgambo JKT [Sheikh Amri Abeid, Arusha]
Simba v Tanzania
Prisons [National Stadium, Dar Es Salaam]
Septemba
30.
Yanga v African
Lyon [National Stadium, Dar es Salaam]
Oktoba 1 .
Ruvu Shooting v
Mtibwa Sugar [Azam Complex, Dar es Salaam]
Oktoba 3 .
African Lyon v
Toto Africans [Azam Complex, Dar es Salaam]
Ruvu Shootings v
Kagera Sugar [Mabatini, Pwani], Pwani]
JKT Oljoro v
Coastal Union [Sheikh Amri Abeid, Arusha]
Yanga v Simba
[National Stadium, Dar es Salaam].
Ligi Kuu
Uingereza matokeo ya Leo Septemba 23..
Ligi Kuu
Uingereza matokeo ya Leo Septemba 23..











No comments:
Post a Comment