Matokeo ya Ligi kuu ya Hispania (Spanish Primera Liga, German Bundesliga na Barclays Premier League). - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 23, 2012

Matokeo ya Ligi kuu ya Hispania (Spanish Primera Liga, German Bundesliga na Barclays Premier League).

Chelsea 1 Stoke 0.


Bao la Dakika ya 85 la Fulbeki Ashley Cole limewapa ushindi wa bao 1-0 Chelsea wakiwa kwao Stamford Bridge na Stoke City na kuendelea kutinga kileleni mwa Ligi Kuu wakiwa na Pointi 13 baada ya Mechi 5.


Southampton 4 Aston Villa 1.

Baada ya vichapo mfululizo tangu Msimu uanze leo Southampton wamezinduka na kuitandika Aston Villa bao 4-1.

Aston Villa ndio waliotangulia kupata bao katika Dakika ya 10 ambalo alifunga Darren Bent na kudumu hadi mapumziko.

Kipindi cha Pili Southampton wakapiga bao 4 kupitia Rickie Lambert, Dakika ya 58 na 90 kwa Penati na Clyne, Dakika ya 63 na 65.


Wigan 1 Fulham 2.

Bao za Hugo Rodallega, Dakika ya 32, na Damien Duff, 68, zimewapa Fulham ushindi wa ugenini wa bao 2-1 walipocheza na Wigan ambao bao lao moja lilifungwa na Kone katika Dakika ya 90.



West Bromwich Albion 1 Reading 0.

Bao la Dakika ya 71 la Lukaku limewapa ushindi WBA wa bao 1-0 dhidi ya Reading.

West Ham 1 Sunderland 1.

Wakiwa kwao Upton Park, West Ham leo waliokolewa na Nahodha wao Kevin Nolan ambae alisawazisha bao katika Dakika ya 90 na kwenda sare ya 1-1 na Sunderland waliotangulia kupata bao katika Dakika ya 10 mfungaji akiwa Steven Fletcher.


Aidha ligi hiyo soka Uingereza kwa jumapili hii ni BIGI MECHI kati ya  Liverpool v Man United

[Saa 9 na Nusu Mchana] & Man City v Arsenal

[Saa 12 Jioni]




MANCHESTER CITY

Hart
Maicon, Kompany, Lescott, Clichy
Garcia, Barry
Milner, Toure, Silva
Tevez
ARSENAL

Mannone
Jenkinson, Mertesacker, Vermaelen, Gibbs

Arteta, Cazorla, Diaby

Oxlade-Chamberlain, Gervinho, Podolski







Man City wanatoka kwenye kipigo cha 3-2 huko Santiago Bernabeu mikononi mwa Real Madrid kwenye UEFA CHAMPIONZ LEAGUE na Arsenal kwenye wimbi la ushindi, kwanza walipoitandika Southampton 6-1, na kisha ugenini 2-1 walipoifunga Montpellier.
 

Uso kwa Uso.


Man City wameifunga Arsenal katika Mechi 4 kati ya 5 walizocheza mwisho nyumbani kwa City na katika Mechi 4 za mwisho walizokutana, Kadi Nyekundu 4 zimeshatembezwa na 3 zilikuwa kwa Wachezaji wa Man City.


LIVERPOOL

Reina
G. Johnson, Agger, Skrtel, Enrique
Allen, Gerrard, Shelvey
Borini, Suarez, Sterling
  MANCHESTER UNITED

De Gea
Rafael, Ferdinand, Vidic, Buttner

Carrick, Scholes

Valencia, Kagawa, Nani
Van Persie




Mchezo huu unachezwa  wakati Liverpool wamekumbushwa majonzi ya msiba wa Mashabiki wao 96 kwenye maafa ya Mwaka 1989 huko Hillsborough kwenye Mechi ya Nusu Fainali ya FA Cup kati ya Liverpool na Nottingham Forest na pia lile sokomoko la Mchezaji wao Luis Suarez kukataa kumpa mkono Beki wa Man United Patrice Evra.
 


 Wiki nzima hii, Viongozi wa Klabu hizo mbili wamekuwa wakijitahidi kuwaomba Mashabiki wa pande zote mbili kuheshimiana ambapo katika Barua ya Ferguson ambayo Mashabiki wa Manchester United watapewa huko Anfield kabla ya kuingia Uwanjani amewakumbusha kuwa Man United “inasimama pamoja na Liverpool.’’


Msimu huu Liverpool wana matatizo ya ufungaji na wanaingia kwenye Mechi hii wakiwa na mwendo wa kusuasua kwenye Ligi lakini pia Difensi ya Manchester United inaonyesha dalili za kuyumba.

 

Msimamo wa Timu za Juu:



Na     Team          Points         Games
1.       Chelsea          13                 5
2.       Everton          10                 5
3.       West Brom    10                 5
4.       Fulham            9                 5
5.       Man. United    9                4
6.       Arsenal             8                4
7.       Man. City         8                4
8.       West Ham        8                 5
9.       Swansea            7                5
10.    Tottenham         5                4





Matokeo ya Ligi kuu ya Ujerumani (German Bundesliga


RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Septemba 21.

Nuremberg 1 Eintracht Frankfurt 2

Jumamosi Septemba 22.

Schalke 0 Bayern Munich 2

VfL Wolfsburg 1 Greuther Fuerth 1

Mainz 05 2 Augsburg 0

Hamburg 3 Borussia Dortmund 2

Fortuna Duesseldorf 0 Freiburg 0

Jumapili Septemba 23.

Bayer Leverkusen v Borussia Moenchengladbach

Werder Bremen v VfB Stuttgart

Hoffenheim v Hanover 96




Matokeo ya Ligi kuu ya Hispania  (Spanish Primera Liga




RATIBA==LA LIGA:
Jumamosi Septemba 22 
 
Real Zaragoza 3 v Osasuna 1

Celta de Vigo 2 v Getafe 1

Real Betis 1 v RCD Espanyol 0

FC Barcelona 2 v Granada CF 0

Jumapili Septemba 23

13:00 Real Mallorca v Valencia

17:00 Levante v Real Sociedad

19:00 Atletico de Madrid v Real Valladolid

20:50 Athletic de Bilbao v Malaga CF

22:30 Rayo Vallecano v Real Madrid CF

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad