Mkuu wa
Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas E Mwangela akikagua ujenzi wa daraja
la Kikamba linalounganisha kata ya Kapalala na Gua Wilayani Songwe, katika
ziara yake ya siku mbili wilayani humo aliyoianza leo. Daraja hilo limeanza
kujengwa Oktoba 20, 2017 na linatarajiwa kukamilika Septemba, 2018 likiwa
limegharimu shilingi bilioni 1.4.
Na Grace
Gwamagobe - Songwe.
Mkuu wa Mkoa
wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Mwangela amekataa ombi la Mkandarasi
kutoka kampuni ya Mats Engineering Ltd Paulo Philipo Paulo la kuongezewa
kipindi cha miezi miwili ili aweze kukamilisha ujezi wa Daraja la Kikamba
Wilayani Songwe.
Brigedia
Jenerali Mwangela amekataa ombi hilo leo alipokagua ujenzi wa daraja la Kikamba
linalounganisha kata za Kapalala na Gua wilayani Songwe kwakuwa sababu alizotoa
mkandarasi huyo hazijitosheleji.
Amesema
daraja hilo lazima likamilike kwa muda uliopangwa ambao ni Septemba, 2018 huku
mkandarasi huyo akitoa sababu kuwa atachelewa kukamilisha ujenzi huo kutokana
na mvua nyingi zilizonyesha na mwamba mgumu uliopo eneo la ujenzi.
“Mkandarasi
ahakikishe anafanya kazi mchana na usiku ili akamilishe ndani ya muda wa
mkataba, vifaa vya kumuwezesha kufanya hivyo anavyo na ombi la kuongezewa muda
wa ujenzi mimi siafikiani nalo”, amesema Brigedia Jenerali Mwangela.
Naye Mkuu wa
Wilaya ya Songwe Samuel Jeremia amesema yeye na viongozi wengine wataendelea
kusimamia miradi ya maendeleo na katika ujenzi wa daraja hilo watahakikisha
wanamsimamia mkandarasi huyo ili amalize ndani ya muda uliopangwa.
Daraja la
Kikamba linaolunganisha kata za Kapalala na Gua limeanza kujengwa mwezi Oktoba
2017 na linatarajiwa kukamilia Septemba 2018 likiwa limegharimu shilingi
bilioni 1.4.
|
Thursday, August 16, 2018
![](https://1.bp.blogspot.com/-7Kd9qaiRHuA/WaEtZyc70TI/AAAAAAAADsA/7WUYBVoY-UwwjdEP3kDFPvH9htN0dDKgQCLcBGAs/s1600/demo-image.jpg)
RC Songwe- Akataa Ombi la Mkandarasi Kuongezewa Muda.
Tags
# MATUKIO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MATUKIO
Labels:
MATUKIO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment