Mfanyabiashara
wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma Bw. Eliya Ntinyako, akitoa malalamiko
yake kuhusu adhabu aliyopewa baada ya mashine ya kutolea Lisiti za
Kielektroniki- EFDs kuharibika wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani), na wafanyabiashara wa
Manispaa hiyo.
Aidha Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda na
Kilimo Tanzania (TCCIA), Mkoani Kigoma, Bw. Prosper Guga, alisema kuwa matatizo mengine yanayodhoofisha
biashara na kudidimiza uchumi wa Mkoa wa Kigoma unaopakana na Nchi ya Burundi
na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni kutokuwepo kwa Benki
za Kimataifa hususani nchini DRC jambo linalowafanya wafanyabiashara kutembea
na fedha taslimu hivyo kuwa hatari kwa usalama wa fedha hizo kwa kuzingatia
mazingira ya nchi wanzaofanyanazo biashara.
“Wizara ya Fedha na Mipango isaidie kuzishawishi Benki za
Biashara kufungua matawi katika nchi za DRC, Burundi na nyingine ili kukuza
zaidi biashara katika ukanda huu ambao una fursa kubwa za biashara”
aliongeza Bw. Guga.
|
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu
Kijaji (Mb) (wa pili kulia), akiwaeleza wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma
Ujiji umuhimu wa kutoa lisiti na kulipa kodi, wakati changaoto za biashara na
nchi jirani zikitatuliwa, alipofanya Mkutano na wafanyabiashara wa Manispaa
hiyo Mkoani Kigoma, wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Rashid
Kassim Mchatta na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi. Mwanamvua Mlindoko.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu
Kijaji (Mb) (wa pili kulia), akiwaeleza wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma
Ujiji umuhimu wa kutoa lisiti na kulipa kodi, wakati changaoto za biashara na
nchi jirani zikitatuliwa, alipofanya Mkutano na wafanyabiashara wa Manispaa
hiyo Mkoani Kigoma, wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Bw. Rashid
Kassim Mchatta na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi. Mwanamvua Mlindoko.
|
Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Elijah Mwandumbya, akifafanua taratibu za ukadiriaji wa kodi ambapo aliwataka wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za lisiti ili iwe rahisi kwa mtumishi wa Mamlaka hiyo kukadiria kodi bila malalamiko, kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wfanyabiashara wa Mkoa wa Kigoma Bw. Juma Chaurembo, na kushoto ni Afisa Biashara wa Mkoa huo Bw. Deogratias Sangu. |
Kamishna wa
Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA) Bw. Baghayo Saqware, akitoa elimu kwa
wafanyabiashara wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma kuhusu umuhimu wa
Bima wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Ashatu Kijaji (Mb) na wafanyabiashara hao.
Mbunge wa
Kigoma Mjini Mhe. Zito Kabwe, akitoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya Kodi
zinazotozwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji wakati wa Mkutano kati
ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili
kushoto) na wafanyabiashara wa Manispaa hiyo.
Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, ameishauri Serikali kuufanya
mji wa Kigoma kuwa Bandari Kavu ili mizigo yote inayosafirishwa kwa treni
kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kwa ajili ya kuivusha kwenda nchi jirani za
Congo na Burundi, ianzie katika mji huo wa kibiashara ili kukuza ajira na
uchumi wa mkoa huo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji alisema kuwa amefurahishwa na hoja za
wafanyabiashara hao hivyo akaahidi kushirikiana na Wizara nyingine ikiweo ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki na pia Wizara ya Mambo ya Ndani ili kulipatia ufumbuzi suala hilo kwa
haraka.
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya
Congo mwaka 1991/92 walikubaliana kuwa na soko na mahusiano mema
kati ya Mkoa wa Kigoma na mikoa jirani ya Congo, lengo likiwa wafanyabiashara
hao kuuza bidhaa Kigoma na kununua bidhaa na mazao kwenda Congo hivyo
kurahisisha wafanyabiashara wadogo kufanyabiashara na kuibua matajiri wakubwa
katika kipindi cha mwaka 1990 hadi 2000.
|
No comments:
Post a Comment