Mfano wa Choo Bora.
Jumla ya
kaya 604 Wilayani Ngara Mkoani Kagera hazina Vyoo Bora kutokana na takwimu
zilizo patikana baada ya Kampeni ya Choo ni Nyumba iliyofanyika kwa Usimamizi wa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo.
Akizungumza
na Radio Kwizera Bw Aidan Bahama amesema viongozi wote kuanzia ngazi
ya shina mpaka tarafa wafuatilie na kubaini nyumba ambazo hazina vyoo
ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa choo.
Aidha
amewataka viongozi wote kuanzia mabalozi kuorodhesha kaya ambazo hazina choo na kuahidi
kuzisaidia familia ambazo hazina uwezo wakujenga choo kutokana na matatizo
mbalimbali.
Naye Mratibu
wa Kampeni ya kitaifa ya Usafi wa Mazingira wilayani Ngara Bw Mansour Kalokola
amewataka watendaji wa vijiji na kata kuandika majina kwenye
madaftari yaliyo tolewa kwa ajili ya takwimu ili ziweze kufanyiwa kazi.
|
No comments:
Post a Comment