![]() |
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Salum M. Kijuu akimkabidhi ilani ya chama cha CCM,Katiba Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani humo Michael Mtenjele mara baada ya kumuapisha.
Na: Sylvester Raphael.
Mambo kumi muhimu aliyoyafanya na atakumbukwa nayo kama alama ya utawala wake wa miaka miwili na siku 140 kama Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli Machi 13, 2016 na kushika kijiti cha kuiongoza Kagera hadi Julai 28, 2018 alipostaafu.
Ulinzi na Usalama:
Ikiwa ni ahadi yake mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera Mhe. Kijuu wakati akikabidhiwa ofisi na Mtangulizi wake John Mongella Machi 22, 2016 alisema kuwa ujambazi Kagera ungekuwa historia na kweli tangu wakati huo mkoa umekuwa shwali wananchi wakitekeleza shughuli zao za kujenga uchumi bila matukio makubwa ya kutisha ya ujambazi kama hapo awali.
Tetemeko Septemba 10, 2016:
Mara baada ya Mkoa wa Kagera kukumbwa na Janga la Tetemeko lililotokea Septemba 10, 2016 na kuua watu 17, kujeruhi watu 253, nyumba 840 kuanguka na nyumba 1,264 kupata nyufa Mhe. Kijuu alikuwa mstari wa mbele kuwafariji wananchi wote waliopatwa na janga hilo.
Wakati wa
Tetemeko Mhe. Kijuu alisimamia
kidete matibabu ya majeruhi ili kupata tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Kagera pamoja na vituo vingine ambavyo vilikuwa vinatoa huduma kwa wahanga
wote.
Aidha, alihakikisha
kuwa taratibu zote za kuwahifadhi wananchi waliopoteza maisha yao zinakamilika
kwa kugahrimiwa na Serikali ikiwa ni pamoja na kutoa rambirambi kwa familia
zilizopoteza wapendwa wao.
Baada ya
Tetemeko Mhe. Kijuu alisimamia
ipasavyo Akaunti ya Maafa iliyoanzishwa kwa ajili ya wadau mbalimbali kuchangia
maafa ikiwa ni pamoja na kuongoza Kamati ya Maafa Kagera ikiundwa na Mkoa
kwakushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha Maafa ambapo jukumu kubwa
ilikuwa ni kuratibu michango mbalimali na kuidhinisha matumizi ya michango hiyo
na kusimamia urejeshwaji wa hali baada ya Tetemeko kutokea.
Kupitia
usimamizi wake mzuri baadhi ya wananchi waliokuwa hawajiwezi kama wazee
walipatiwa vifaa vya ujenzi kama saruji, misumari, mabati, nguo chakula na
vifaa vinginevyo.
Pia Mhe. Kijuu alisimamia vizuri ujenzi
mpya wa Shule ya Sekondari Ihungo na Nyakato na Ukarabati wa Shule ya Sekondari
Omumwani Manispaa ya Bukoba, Kituo cha Afya Kabyaile Wilayani Missenyi,
Ukarabati na Upanuzi wa Kituo cha Afya Kayanga Wilayani Karagwe.
|
![]() |
John Mongela sasa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,akimkabidhi Ofisi
rasmi na Mtangulizi wake Mhe. John Mongella Machi 22, 2016.
|
![]() |
Operesheni Ondoa Mifugo
Kagera:
Tarehe 18 Machi, 2018 Mhe. Kijuu alitoa siku tatu kwa wavamizi wote wa Misitu ya Hifadhi na Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi na Kimisi ambapo mara baada ya siku hizo kuisha iliendeshwa Operesheni kali ya kusafisha mapori hayo na misitu ya hifadhi na kufanikiwa kuondosha zaidi ya mifugo 14,000 ikiwa ni pamoja na kuondosha wahamiaji haramu wote katika Mapori hayo.
Kutokana na
mafanikio makubwa ya operesheni hiyo iliyosimamiwa na Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu akiwa Mkuu wa Mkoa wa
Kagera wanyama wengi waliweza kurejea kwa kasi sana na sasa Serikali imetangaza
Mapori hayo kuwa Hifadhi za Taifa. Asante Mhe. Kijuu.
Huduma za Madaktari Bingwa
Kagera:
Ikiwa ni
ahadi yake wakati akikabidhiwa ofisi alipowasili Mkoani Kagera kusimamia
ukusanyaji wa mapato ya Serikali alifanikiwa kusimamia Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Kagera kukusanya mapato ya kutosha na kufanikiwa kuleta Madaktari
bingwa kwa fedha za ndani za hospitali hiyo baada ya kufunga mifumo ya
ukusanyaji wa mapaton.
Madaktari
hao Bingwa waliweza kutoa huduma za kibingwa kwa wagonjwa 3,146 kati ya 5,700
waliojitokeza kupata huduma.
Katika zoezi
hilo lililoendeshwa kwa siku 10 tangu Septemba 18 hadi 28, 2017 Madaktari
Bingwa walilipwa kwa fedha za ndani na zilikusanywa kiasi cha shilingi milioni
34,886,3338/=.
Aidha, Fedha hizo pia ziligharamia ununuzi wa madawa na vifaa
tiba vilivyotumika katika zoezi.
Kilimo:
Mhe. Kijuu akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliweza kuhamasisha wananchi kila mara alipopata fursa kuhusu kilimo. Alianzisha kampeini ya kila familia kupanda miche ya miti ya matunda mitano kupambana na utapiamlo.
Pia
aliwahamasisha vijana kuunda vikundi na yeye kuwasaidia kuwapatia matrekta ya
kulima mashamba makubwa ili waweze kunufaika na kilimo.
Magendo ya Kahawa:
Kutokana na Serikali kuanzisha mfumo mpya wa ukusanyaji na uuzaji wa kahawa ya wananchi Kagera kupitia Vyama vya Ushirika Mhe. Kijuu alisimamia kidete kuhakikisha hakuna mwanachi yeyote atakayeuza kahawa kimagendo kwa njia ya obutura.
Maono yake
yalikuwa ni kumuona mkulima akinufaika na kilimo chake bila kuibiwa au kulipwa
kiduchu kwa kulaghaiwa na wafanyabiashara.
Elimu:
Mhe. Kijuu alisimamia upatikanaji wa madawati katika shule za Sekondari na Msingi, pia alisimamia agizo lake la kuhakikisha kila Halmashauri inakuwa na Shule moja ya kidato cha tano na sita ambapo shule kama Kagemu, Omumwani Manispaa ya Bukoba zilianzishwa, Nyailigamba Muleba, na Murusagamba Ngara zilianzishwa wakati wa utawala wake Mhe. Kijuu.
Afya za Watumishi na
Wananchi:
Mhe. Kijuu alianzisha utaratibu wa watumishi pamoja na wananchi wote kufanya mazoezi kila siku ya Jumamosi kila wiki ili uboresha afya zao na kuweka miili yao sawa ili kuepukana na magonjwa nyemelezi. |

![]() |
Ushirikianao na Vyombo vya
Habari:
Mhe. Kijuu alikuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Vyombo mbalimbali Vya habari ikiwa ni pamoja na Waandishi wa Habari bila kujenga matabaka kati yao. Aliwathamini Waandishi pamoja na Vyombo vyao na kazi zao kwa ujumla katika kuhakikisha habari za Mkoa wa Kagera zinasikika ndani na nje ya Mkoa.
Utalii:
Mara baada ya kukamilisha operesheni ya kuondoa wavamizi na mifugo katika Misitu ya Hifadhi na Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi na Kimisi na Serikali kutangaza Mapori hayo kuwa Hifadhi za Taifa Mhe. Kijuu alikuwa ameanza kwa kasi sana kuwahamasisha wananchi wa mkoa wa Kagera kuchangamkia fursa za utalii katika maeneo hayo.
Meja
Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuuumetumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania miaka 40 pia umeongeza miaka miwili na
siku 140 za kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Kagera, tunashukuru kwa huduma yako
na utumishi uliotukuka.
|
![]() |
Kagera umetuacha salama tukiwa wamoja kati ya Serikali ya Mkoa na Wananchi wake pia tutaendelea kuyaenzi mazuri yako. Tunasema kwaheri na Karibu tena Kagera ni nyumbani kwako. Tunakutakia mapumziko mema na Mwenyezi Mungu aendelee kukulinda ukiwa na afya njema. |
No comments:
Post a Comment