Inahuzunisha- Mwili waanza Kuoza kwa Kukosa Msaada wa Matibabu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 24, 2018

Inahuzunisha- Mwili waanza Kuoza kwa Kukosa Msaada wa Matibabu.

Vijana wakazi wa kijiji cha Murukukumbo wilaya ya   Ngara mkoani Kagera wakiwa nje baada ya waandishi wa habari na mtawa kuingia ndani kumuona mgonjwa ndani ya nyumba hiyo ndimo anamoishi tangu apate ajali. 

Na:Shaaban Ndyamukama –Ngara.

Mgonjwa aliyepata ajali ya kuamguka katika shimo la  choo na kukatika uti wa mgongo mkazi wa  kijiji cha Murukukumbo Kata ya Kabanga wilaya ya   Ngara mkoani Kagera, kisha kukosa fedha za matibabu mwili wake umeanza kutoa wadudu baada ya kuoza sehemu za nyonga. 

Mkazi huyo Gwasa Jacob (40) alipata ajali akiwa Mutukula wilayani Misenyi Februari mwaka huu,2018 na kufikishwa hospitali ya rufaa ya  mkoa wa Kagera lakini alitakiwa kwenda  kutibiwa hospitali ya Bugando na familia kukosa fedha.  

Akizungumza na waandishi wa habari July 23, 2018 alisema alitelekezwa na ndugu zake na sasa naishi ndani ya yumba akiwa peke yake .

Aidha wanaokuja kumuona wanaacha wamemfungia na hana chakula na kwamba anachokihitaji hakipati kutoka kwa ndugu zake.
Mgonjwa akiwa amelalani Ndani.

Mgonjwa huyo amelazwa kwenye nyumba iliozeeka ambayo iliachwa na mama yake aliyefariki miaka kadhaa sasa, imejengwa kwa udongo, analala kwenye jamvi la makuti ya migomba akiwa na blanketi ambalo ni chafu lililoshikana na nyama za mwili wake.

Francisco Kitulu ambaye ni Mwenyekiti wa ukoo wa  ABAVUMU alisema  mgonjwa huyo alitelekezwa na ndugu zake baada ya kuwataka wauze shamba kupata fedha kumsafirisha hadi hospitali ya Bugando lakini wao walikataa  na kujiingiza kwenye matibabu ya waganga wa kieyeji.

Alisema sehemu ya shamba iliyouzwa waliitafuna kwa kunywa pombe  na kiasi kingine kumpelekea mganga wa miti shamba lakini hali ni mbaya kwani sehemu ya nyonga inaonekana mifupa baada ya nyama za mwili kushmbuliwa na wadudu. 
Waandishi wa habari wakiwa nje ya nyumba alikolala Mgonjwa.
 
Mwenyekiti wa kijiji cha Murukukumbo Simon John alipoulizwa  kuhusu mgonjwa uyo alisema anazo taarifa zake lakini alijua wanaukoo na familia wanamuuguza hivyo hakuwai kupata malalamiko ya mgonjwa kutelekezwa.

Majirani na watu wengine katika kijiji hicho walisema tangu kuugua kwake  kijana huyo Gwassa Jacob hawakushirikishwa na ndugu zake  au viongozi ili apelekwe hospitali kwani wangetoa michango yao  kumpatia chakula na mahitaji mengine. 
Gwassa Jacobo aliondoa kijiji cha Mulukuumbo akielekea wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera, kutafuta maisha  na kumpata mke aliyezaa naye watoto wawili mmoja wao  ana umri wa miaka minane alipata naye ajali mwezi februari kweye shimo la choo na kupata majeraha ya kawaida.

Inasemekekana wakati akipata matibabu katika hospitali ya mkoa wa Kagera alijitokeaza msamalia mwema  abaye hakujulikana aliyemchukua mtoto wake wa kiume   kwenda kuishi naye akidai atamsomesha shule ya msingi.

Oliva Niyonzima ambaye ni Mtawa  kutoka Shirika la Masister wa Francisco wa Mt. Bernadetha Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara alifika  ndani ya nyumba alikolala mgonjwa huyo baada ya kumfunua alikuta mwili ukitoka wadudu na harufu kali.

Niyonzima  aliwaomba Wananchi kujawa na moyo wa huruma kujitokeza kumaiidia kwa kumuondoa kwenye nyumba allikolazwa na kumpeleka sehemu yenye usalama ili asijekudhuliwa na mbwa wa usiku.

Waandishi wa habari walioungana na Sister Oliva Niyonzima alishauri wananchi na viongozi pia wanaukoo kumfuatilia mgonjwa huyo na kumpatia huduma kama chakula na kufanya usafi wa mwili wake kisha kumfikisha Hospitali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad