![]() |
Tembo wakila .Picha na Maktaba
Yetu.
Tembo Wapatao
25 wakitokea katika Msitu wa Hifadhi wa Kimisi,mkoani Kagera wamevamia kitongoji cha Kamuli, Kata ya Kasulo
wilayani Ngara Mei 10, 2018, na kuharibu mazao ambayo thamani yake haijajulikana
bado.
Akiongea kwa
njia ya simu Afisa Mtendaji wa Kata ya Kasulo Bw. Peter Jeremiah Kapalala, amesema Tembo hao walivamia mashamba
usiku wa kuamukia Alhamisi, na kuharibu mashamba ya Mahindi, Karanga na
Maharage.
“Wananchi wamejitahidi kuwafukuza tembo hao,
ili warejeetena katika pori la hifadhi, lakini imetuchukua muda mrefu, kwani
hadi saa tano asubuhi walikuwa bado wamo mashambani.” Alisema Mtendaji Kapalala.
Insemekana
wanyama hao hawakuwadhuru watu na wala watu hawakuwadhuru tembo hao, na kwamba
pamoja na kuwafukuza inaonekana wanyama hao hawakwendambali, na wananchi wana
wasiwasi kwamba uenda wakarejea tena.
|
Saturday, May 12, 2018

Tembo Wafanya Uharibifu wa Mazao Kijijini Kamuli,Kasulo-Ngara.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment