![]() |
Afisa Elimu
Msingi Halmashauri ya Sengerema Bw.Oscar
Kapinga amesema kuwa baada ya vitabu hivyo kufika mashuleni walimu watapata nafasi nzuri ya kuwafafanulia wanafunzi kwa kuwa kila mwanafunzi atakuwa na kitabu chake. hata hivyo, Katika taarifa iliyosomwa na Mwl.Tema Heri kwa niaba ya Mkuu wa shule ya Msingi Pambalu Bi.Sundi Mussa kwa Mkuu wa wilaya ya Sengerema imeeleza kuwa shule hiyo haijapokea kitabu hata kimoja cha mtaala mpya wa darasa la nne na kwamba ufundishaji katika darasa hilo mpaka sasa ni wa kusua sua kutokana na kwamba mtaala unaotumika kufundishia wanafunzi wa darasa la nne ni wa zamani ambao sasa umepitwa na wakati. |
![]() |
Mkuu wa wilaya hiyo Bw.Emmanuel
Kipole amesema kuwa changamoto hiyo
inafahamika Serikalini na mkakati wa kuitatua na kuimaliza kabisa unaendelea.
Imeelezwa kuwa kupatikana kwa vitabu vya darasa la
kwanza hadi la tatu kumemaliza kabisa changamoto ya wanafunzi sita kutumia kitabu kimoja ambapo kwa sasa serikali imetimiza mpango wa kitabu kimoja kutumika kwa mwanafunzi mmoja. |
No comments:
Post a Comment