





![]() |
Kufuatia Sakata
hilo, Kamishna wa huduma kwa mteja na sheria wa idara ya uhamiaji makao makuu
nchini Anolile Manyaga aliwaomba
radhi wananchi katika mkutano wa hadhara baada ya kufanyika kikao cha ndani kusikiliza
malalamiko ya walio fanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kuonewa.
Manyaga alisema hatua za kinidhamu
zitachukuliwa kwa maafisa hao kwani wamechafua idara lakini wananchi waendelee
kutoa ushirikiano katika kuwaondoa wahamiaji haramu nchini na kwamba taratibu
za utumishi zitatumika kuwawajibisha watakaobainika kujihusisha na vitendo
hivyo.
Maafisa uhamiaji watano wanaotuhumiwa kufanya uhalifu katika
mji wa Kabanga wamefikishwa mahakama ya wilaya wakituhumiwa kutenda kosa la
jinai kwa kuvunja kifungu cha sheria namba 241 sura ya 16 ya mwaka 2002.
Hata hivyo watuhumiwa walikana shitaka
linalowakabili ambapo wamepata dhamana mpaka May 12 mwaka huu.
|
![]() |
Picha na -Radio Kwizera Ngara. |
No comments:
Post a Comment