Mwenyekiti
wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila
(Kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa ufafanuzi kuhusu
malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd,
Leo 7 Aprili 2018, Mwingine ni Kaimu meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha ushirika
cha Kagera (KCU) Ndg John kanjagaile. Picha Zote Na Mathias Canal, WK.
Na Mathias
Canal, WK-Dodoma.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila ametoa
ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera
KCU (1990) Ltd kama ilivyojadiliwa kwenye Mkutano wao Mkuu tarehe 27/03/2018.
Amebainisha
hayo wakati akizingumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Mjini Dodoma na
kusema kuwa Chama Kikuu cha Ushirika cha Kagera si Kampuni ya kununua kahawa
bali ni ushirika wa wakulima wadogo wadogo wenye lengo la kuunganisha nguvu zao
kwa pamoja katika kuhudumia zao la kahawa na kuliwasilisha sokoni kwa utaratibu
wenye tija endelevu na kisha kugawana mapato
baada ya kufanya mauzo.
Alisema bei
halisi ya mkulima kwa upande wa Ushirika inapatikana mara baada ya mauzo ya
kahawa kufanyika ambapo wakulima hulipwa
malipo ya mwisho kwa kadri ya bei ya kuuzia iliyopatikana sokoni na hesabu ya
mwisho kuwasilishwa kwenye mkutano mkuu.
Hivyo kwa
vile mchakato wa mauzo huchukua si chini ya kipindi cha mwezi mmoja tangu
mkulima awasilishe kahawa yake kwenye ushirika hadi malipo ya mwisho kufanyika,
basi ili kumuondolea mkulima adha ya kusubiri malipo yake yote baada ya mauzo
wakati anahitaji kujikimu na kukidhi mahitaji yake muhimu, wakulima wenyewe kwa
utashi wao kupitia Mkutano Mkuu,
wanajadili malipo ya awali atakayotanguliziwa mkulima wakati anasubiri malipo
ya mwisho.
|
Waandishi wa
habari wakifatilia Mkutano wa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika
cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya
awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd, Leo 7
Aprili 2018, Katika Ukumbi wa Ofisi za Wizara ya Kilimo (Kilimo 4).
Niyegila
alibainisha kuwa mnamo tarehe 27/03/2018, Chama Kikuu cha Kagera kilifanya
Mkutano wake Mkuu ambao pamoja na mambo mengine wanachama walijadili malipo ya
awali ya mkulima (Advance Payments).
Katika makisio hayo, Menejimenti na Bodi ya KCU (1990) Ltd
walipendekeza malipo ya awali yawe ni TZS 1,000 kwa kilo moja ya kahawa ya
maganda.
Alisema kuwa
baada ya mjadala, wanachama waliagiza kupitiwa upya kwa makisio hasa katika
upande wa malipo ya awali na kuangalia namna ya kupandisha kiwango cha malipo
ya awali.
Aliongeza kuwa Kiwango kipya pendekezwa kitawasilishwa kwa Mrajis wa
Vyama vya Ushirika nchini kwa ajili ya kuidhinishwa.
Alisisitiza
kuwa kile kilichojadiliwa kwenye Mkutano Mkuu wa wanachama si tangazo la bei
bali ni malipo ya awali kwa mkulima ambapo Kwa mujibu wa sheria, bei elekezi ya
zao la kahawa inatolewa na Bodi ya Kahawa Tanzania kwa utaratibu wa ushirika,
bei halisi itajulikana mara baada ya mauzo ya kahawa kufanyika sokoni na si
vinginevyo.
Niyegila
aliongeza kuwa kwa utaratibu wa sasa wa Serikali, kahawa yote itakusanywa
kupitia kwenye Vyama vya Ushirika na kupelekwa sokoni Manispaa ya Moshi Mkoani
Kilimanjaro ambapo wanunuzi wote watanunulia hapo mnadani.
Kwa mantiki
hiyo, hakuna mkulima yeyote atakayeruhusiwa kuuza kahawa nje ya mfumo wa
ushirika.
|
No comments:
Post a Comment