Spika wa
Bunge, Job Ndugai ametaka kina mama wenye malalamiko ya kutelekezewa watoto na
wabunge wafike kwake au wamwandikie barua kuhusu suala hilo.
Hata hivyo,
amesema watakapofanya hivyo wapeleke na cheti cha uthibitisho cha vipimo vya
vinasaba (DNA) ili waone ni namna gani ya kushughulikia suala hilo.
Ndugai
alisema hayo Jumanne Aprili 10, 2018 kabla ya kuahirisha kikao cha sita cha
Bunge mjini Dodoma.
Katika kauli
yake iliyoambatana na vicheko Spika alisema, “Kule Dar es Salaam kuna zoezi
linaendelea, huko sasa kidogo kiti cha Spika kimetikiswa hivi. Tunatuhumiwa
mahali, kidogo tumeguswa hivi kwa hiyo natarajia kupata ushauri wenu
waheshimiwa tunafanyaje katika mazingira haya kwa maana kuna watoto wetu wako
barabarani.”
“Haiwezekani
hata kidogo, kwa hiyo kina mama wale inabidi tufanye utaratibu tujue nini
tutafanya lakini pia kuna kina baba wamejitokeza huko nimesikia na baadhi ya
walalamikiwa ni kina mama wabunge, kwa hiyo hili jambo halina upande,” alisema
Ndugai.
“Hawa kina
mama kama wapo, basi waje kwa spika au wamwandikie spika lakini waniletee na
DNA test certificate (cheti cha uthibitisho cha vipimo vya vinasaba) ili tuone
namna gani ya kuwezesha.
“Kuna
mafungu hapa tumepitisha tunaweza kuangalia namna ya kuweka sawasawa ili
waheshimiwa wabunge wawe na utulivu katika kufanya kazi za Bunge na si kuwa na
mawazo mengine,” alisema.
Wanawake na
wanaume wamekuwa wakijitokeza katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
kuwasilisha malalamiko kuhusu kutelekezewa watoto.
Akizungumzia
suala hilo jana Aprili 10, 2018 mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda alisema kati ya
wanawake 480 waliosikilizwa 47 walidai wametelekezwa na wabunge.
|
Thursday, April 12, 2018
Spika wa Bunge na Sakata la Wanawake Waliotelekezwa.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment