Shirika la
ugavi wa nishati ya Umeme Nchini TANESCO limeiunganisha wilaya ya Ngara mkoani
Kagera katika Grid ya Taifa na kubadili mfumo wa uendeshaji kutoka matumizi ya
mashine za dizeli kwenda Umeme wa kawaida.
Akizungumza
katika uzinduzi wa kuunganishwa katika Gridi ya Taifa wilayani Ngara, Waziri wa
Nishati Dkt.Medard Kalemani ameeleza
kuwa hatua hiyo itachochea kasi ya maendeleo ya viwanda na kuondokana na
Matumizi ya mafuta ya dizeli ambayo yanagarimu kiasi cha shilingi Milioni 236
kila mwezi sawa na na bilioni 2.83 kwa
mwaka.
|
Dkt.Kalemani
amesema wilaya hiyo imeunganishwa katika Gridi ya Taifa hali itakayopunguza
matumizi makubwa ya fedha za serikali katika uendeshaji wa mitambo baada ya
kuwa katika matumizi ya mashine zinazotumia dizeli tangu mwaka 2004.
|
Katika
taarifa ya mkoa mkoa wa Kagera kuhusu hali ya nishati ya umeme,Meneja wa
TANESCO mkoani humo Mhandisi Francis Maze amesema mapato ya shirika hilo kwa
mwaka ni shilingi milioni 500 tu,wakati matumizi kwa mwezi ni kiasi cha shilingi Milioni 236 sawa na shilingi bilioni 2.83 kwa mwaka hali ambayo
inakwamisha shughuli nyingi za shirika hilo.
|
No comments:
Post a Comment