Jumla ya
miradi 65 ya maendeleo itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru mkoani Kagera na miradi
miwili ni kati ya miradi 15 ya maendeleo ya mwaka jana 2017 itakakayopitiwa na
Mwenge wa Uhuru kuona uendelevu wake kwa kutoa huduma kwa wamnanchi.
|
Katika
Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Mwenge huo wa Uhuru uliweza kutembelea,
kukagua, kuweka mawe ya msingi Pamoja na kuzindua jengo la kutolea huduma za wagonjwa
wanaoishi na Virusi vya UKIMWI CTC katika Zahanati ya Buhembe Kata Buhembe,
jengo hilo limejengwa na kukamilika pamoja na kuwekewa samani za ndani kwa
gharama ya shilingi 83,626,600/=.
Mara baada
ya kuzindua Jengo hilo Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2018 Charles F.
Kabeho aliwasisitiza wananchi wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kujitokeza kupata
huduma ya matibabu mara baada ya jengo hilo kukamilika.
|
Mwenge wa
Uhuru mwaka huu 2018 umebeba kaulimbiu isemayo “Elimu ni ufunguo wa Maisha; Wekeza Sasa kwa Maendeleo ya Taifa letu.” Kauli mbiu hii inawahamasisha wananchi hususani wa Mkoa wa Kagera kuwekeza katika elimu kwa kuwapeleka watoto shule ili mkoa wetu na Taifa kwa ujumla lipate wataalam wa kutosha katika kada mbalimbali za kitaaluma na hapo taifa letu litapiga hatua kubwa ya maendeleo kwa kuwatumia wataalamu wetu wa ndani. |
No comments:
Post a Comment