Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo akitangaza Majina ya
Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopandishwa Vyeo
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu
jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ameridhia na kuwapandisha
vyeo Maafisa 28 wa Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ kuanzia April 12,2018 huku
akimbadilisha Msaidizi wake Kanali Mbaraka Mkeremy na kumpandisha Cheo.
Katika
taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance
Salvatory Mabeyo, Ikulu Jijini Dar es Salaam amesema Maofisa
walioteuliwa wanakwenda kuimarisha Safu za Utendaji kazi kijeshi na kwamba wote
watavalishwa vyeo vyao April 13,2018 kwenye Makao Makuu ya Jeshi Upanga Jijini
Dar Es Salaam.
Katika
taarifa hiyo,imeeleza kuwa Rais Magufuli
amempandisha cheo Meja Jenarali Peter Paul Massao kuwa Luteni Jenerali.
Meja
Jenerali Massao ni Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa Wanafunzi wa Jeshi Monduli
(TMA) na kwa Uteuzi huo, sasa JWTZ itakuwa na Luteni Jenerali wawili.
Rais
Magufuli amempandisha Cheo pia Brigedia Jenerali, Henry Kamunde kuwa Meja
Jenerali.
Aidha,
Magufuli amewapandisha vyeo Maafisa 27 wa JWTZ kutoka Cheo cha Kanali na kuwa
Brigedia Jenerali na Afisa mmoja kutoka Luteni Kanali na kuwa Kanali.
Waliopandishwa
Vyeo hivyo ni D.D.M Mullugu, J.J Mwaseba, A.S Mwamy, R.K Kapinda, C.D Katenga,
Z.S Kiwenge, M.A Mgambo, A.M Alphonce, A.P Mutta, A.V Chakila, M.G Mhagama, V.M
Kisiri, C.E Msolla na S.M Mzee.
Wengine ni
C.J Ndiege, I.M Mhona, R.C Ng’umbi, S.J Mnkande, A.C Sibuti, M.M Mumanga, I.S
Ismail, M.N Mkeremy, G.S Mhidze, M.A Machanga, S.B Gwaya, P.K Simuli na M.E
Gaguti.
Halikadhalika
Rais Magufuli amempandisha Cheo Luteni Kanali Bernard Masala Mlunga kuwa Kanali
na ameteuliwa kuwa Mpambe wa Rais (Aide
de Camp – ADC)
Kanali
Mlunga ameteuliwa kuwa Mpambe wa Rais akichukua nafasi ya Kanali Mbaraka Naziad
Mkeremy ambaye amepandishwa Cheo kuwa Brigedia Jenerali.
|
No comments:
Post a Comment