Nyavu za Uvuvi haramu Elfu 3 zakamatwa Chini ya Ardhi -Sengerema. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 14, 2018

Nyavu za Uvuvi haramu Elfu 3 zakamatwa Chini ya Ardhi -Sengerema.

Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Sengerema mkoani Mwanza ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Bw.Emmanuel Kipole imefanikiwa kukamata nyavu haramu zaidi elfu tatu mali ya Bw. Joseph Kando mkazi wa Kata ya Nyamatongo zikiwa zimefukiwa chini ya ardhi katika makazi yake pamoja na injin za uvuvi ishirini na sita.

 Akizungumza katika zoezi hilo Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bw.Emmanuel Kipole amesema si mara ya kwanza mtu huyo kukamatwa na zana za uvuvi haramu na zaidi ya awamu tatu amekaa nae ofisini akimsisitiza kuacha kazi hiyo lakin amekaidi na kwamba awamu hii lazima achukuliwe hatua kali za kisheria kwakuwa amekaidi maelekezo na agizo la serikali, lakin pia wakati utaratibu wa kumfungulia mashtaka unaandaliwa jeshi la polisi limeagizwa kumweka ndani kwa masaa 48.

Kwa upande wake kamanda wa oparationi ya kudhibiti uvuvi haramu ndani ya ziwa victoria wilaya ya sengerema Bw.Lesislaus Luhasile amesema kuwa kukamatwa kwa nyavu hizo haramu pamoja na injini ni kutokana na taarifa kiintelenjensia juu ya mtu huyo na kwamba mpaka kumfuata na kumkamata mtuhumiwa huyo tayari walikuwa wanajua ramani ya nyavu zilipochimbiwa na mtuhumiwa amekutwa nyumbani kwake akicheza bao. 
Hata hivyo mtuhumiwa huyo ameamriwa kugharimia gharama za zoezi la ufukuaji wa nyavu hizo zilizo katika mashimo tofauti tofauti ikiwa utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli la kuzuia askari wa Jeshi la Polisi kufanya za aina hiyo. 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad