Mwenge wa
Uhuru umepokelewa leo April 14, 2018 wilayani Ngara Mkoani Kagera na Mkuu wa wilaya
hiyo Luten Kanali Michael Mangwela Mtenjele ukikabidhiwa kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Karagwe Godfrey
Muheluka katika Kijiji cha Rwakalemela ,Kata ya Kasulo ambapo katika Mkoa wa
Kagera Mwenge wa Uhuru umepitia miradi ya maendeleo 65 yenye thamani ya shilingi
bilioni 12,385,330,354.
Mwenge wa
Uhuru mwaka huu 2018 umebeba kaulimbiu isemayo “Elimu ni ufunguo wa Maisha;
Wekeza Sasa kwa Maendeleo ya Taifa letu.”-Na Shaaban
Ndyamukama –Radio Kwizera Ngara.
|
Mkuu wa wilaya ya Karagwe Bw.Godfrey Muheluka akizungumza wakati wa Kukabidhi Mwenge wa Uhuru 2018 wilayani Ngara, amemuahidi kiongozi wa mbio za mwenge Charles Kabeho kuwa ushauri alioacha kwa viongozi na watendaji wilayani humo juu ya miradi yenye changamoto utafanyiwa kazi kwa kufanya marekebisho iweze kuhudumia wananchi. |
Katibu Tawala wilaya ya Ngara, Bw Vedastus Tibaijuka,sambamba na Mkuu wa wilaya hiyo Bw Michael Mtenjele wakati wa utambulisho kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Bw Charles Kabeho.Picha Na Shaaban
Ndyamukama –Radio Kwizera Ngara.
Kiongozi wa
Mbio hizo Charle Francis Kabeho
katika eneo la uwanja wa Kemikimba,Benaco aliwasisitiza Wanafunzi wa Shule ya Msingi na Sekondari
kusoma masomo ya Saysnsi likiwemo somo la Hisabati ili kuweza kupata Wataalamu watakaoweza
kufanya kazi kuinua uchumi wa kati na kupitia sekta ya viwanda.
Kabeho amesema wazazi au walezi wanatakiwa
kuhakikisha wanatoa wahitaji muhimu ya wanafunzi ambayo ni sare ya shule na
vifaa vya darasani ili wajifunze kwa nadhalia na vitendo wakiwa katika
mazingira ya kujifunzia kwa miundombinu iliyopo.
Amesema pamoja na elimu bure kamati za shule
au bodi zitumike kukusanya michango ya kuboresha miundombinu na kuwekeza katika
elimu kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, madawati, vyoo, na ofisi za
walimu lakini michango hiyo isikusanywe na walimu.
"Serikali
imeamua kumpunguzia mzazi au mlezi malipo ya ada kwa shule ya msingi na
sekondari kwa kumuachia jukumu la kumpatia mtoto wake sare na vifaa vya
kujifunzia" Amesema Kabeho.
|
Aidha
amesisitiza jamii kutokomeza ugonjwa wa malaria kwa kuwalinda watoto dhidi ya
ufonjwa huo hasa kwa watoto chini ya miaka mitano na wanawake wajawazito lakini
kujihadhari na UKIMWI kwa kupima afya kwa hiari.
Ameiasa
jamii kupiga vita dawa za kulevya kama bangi na watumie kulimo cha ndizi kwa
chakula na biashara lakini sio kuitumia kwa pombe haramu aina ya gongo, ambayo
ni mojawapo ya dawa za kulevya kwa kughilibu akili za wananchi ambao ni nguvu
kazi ya Taifa.
Katika hatua
nyingine amekemea vitendo vya kutoa na kupokea rushwa ambayo ni adui wa haki na
sio uadilifu kwa mtu kujihusisha na rushwa, hivyo jambo la msingi kila mmoja
awajibike na kutekeleza wajibu na majukumu anayostahili kufanya kisheria.
|
Mkuu wa
wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele amesema Mwenge wa Uhuru 2018 ukiwa
wilayani humo utapitia miradi mitano yenye thamani ya Shilingi Bilioni Sh 2.077
katika Sekta ya Elimu, Afya, Kilimo na Uwekezaji.
|
No comments:
Post a Comment