Unit 55 za Damu Zachangwa na Wananchi wilayani Karagwe. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 14, 2018

Unit 55 za Damu Zachangwa na Wananchi wilayani Karagwe.

Mifuko ya Kuhifadhia Damu baada ya Kutolewa Mwilini mwa Binadamu.

Picha/Habari Na 
Boaz Zobanya,Elen Magambo –Radio Kwizera –Karagwe.

 Jumla ya Unit  55 za damu zimepatikana kutoka kwa Wananchi wakati wa zoezi la kampeni ya uchangiaji  damu kwa hiari April 13,2018 kwenye Viwanja vya Kayanga  wilayani Karagwe mkoani Kagera.

Mkuu wa kidengo Cha Damu  Salama wilayani humo Bi. Abela Bishagi  amebainisha kuwa  zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kwa kukusanya zaidi ya unit 55 za damu ikilinganishwa na Mwaka jana 2017 ambako katika siku kama hiyo walikusanya chini ya Unit 20.

Zoezi hilo lilienda sanbamba na Kampeni ya kuchangia damu inayoendeshwa na Radio Kwizera kupitia kipindi cha Asubuhi Njema yenye kauli mbiu isemayo #DamuYakoMaishaYangu, #DamuYanguMaishaYako.
Mwananchi wa mjini Kayanga,Karagwe mkoani Kagera wakishiriki kuchangia Damu  wakati wa zoezi hilo la Kampeni ya kuhamasisha Watanzania kuchangia damu kwa hiari April 13,2018.

Kituo cha Radio Kwizera cha mjini Ngara  kupitia Kampeni hiyo iliyopewa Jina la DAMU YAKO,MAISHA YANGU  ni waratibu wakuu na itadumu kwa miezi 6 na itafanyika mkoa wa Kigoma na Kagera kwenye wilaya zote. 

Bi Abela amesema  damu hiyo itasaidia wagonjwa wanaopata ajali, watoto wachanga, na akina mama wanaojifungua wakiwemo wa upasuaji katika hospitali na vituo vya Afya wilayani Karagwe.

Wilaya ya Karagwe huhitaji Unit  277 kila mwezi lakini zinazopatikana kwa watu kuchangia damu ni kati ya  lita 70 mpaka 140.

Binadamu ili amchangie mwenzake damu lazima awe na umri wa miaka 18 mpaka 65 na achangie kila baada ya miezi mitatu, awe na afya bila kuwa na magonjwa kama kisukari ambapo siku ya kutoa damu asiwe na ugonjwa wa shinikizo la damu (presha).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad