Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 zinaongozwa na Bw. Charles
Kabeho kutoka mkoa wa Dar es Salaam akishirikiana na Bw.
Issa Abasi Mohamed (Kusini Pemba), Bi. Agusta Safari (Geita), Bw. Ipyana Mlilo
(Tanga), Bw. Dominick Njunwa (Kigoma) na Bi. Riziki Hassan Ali (Kusini Unguja).
Na ukiwa wilayani Ngara utapita Maeneo yenye miradi itakayowekewa
jiwe la msingi na itakayozinduliwa.
Aidha Mkoani
Kagera Mwenge wa Uhuru unakabidhiwa kesho April 8, 2018 wilayani Chato ukitokea
mkoani Geita ambapo wilayani Ngara utapokelewa April 14 na kukabidhiwa
Biharamulo April 15, 2018 kisha April 16, 2018 utaanza kukimbizwa Mkoani
Kigoma.
Mwenge wa
Uhuru 2018 utakimbizwa umbali wa takribani kilomita 103,440.7 kwa siku 195
katika mikoa yote 31 nchini na halmashauri za wilaya 195.
|
Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa vijana sita
watakaokimbiza Mwenge huo,Charles Kabeho wakati alipozindua mbio za Mwenge wa
Uhuru kwenye uwanja wa Magogo mjini Geita, Aprili 2, 2018. Wapili kulia ni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Jenista Mhagama.
|
No comments:
Post a Comment