Mwakilishi
wa Shirika la kuhudumia wakimbizi hapa nchini Bi. Chansa Kapaya, amewashukuru
wafanayakazi wa hospitali za Nyamiaga na Murgwanza katika Halmashauri ya Wilaya
ya Ngara, kwa huduma na ushirikiano walioonesha kwa majeruhi wa ajali ya basi.
Bi. Kapaya
ameyasema hayo Aprili 03, 2018, wakati wa mazishi ya wakimbizi sita walioaga
dunia kwa ajali ya basi, iliyotokea Machi 29, 2018 katika kijiji cha Kasharazi,
wakitokea katika kambi ya wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo mkoani Kigoma na
kuzikwa Benaco Ngara.
Alisema
shirika la kuhudumia wakimbizi, kwa kushirikiana na mashirika mengine,
wamejitahidi kuokoa maisha ya majeruhi, ikiwa ni pamoja na kukodi ndege ya
kuwasafirisha waliopewa rufaa kwenda hospitali ya Bugando.
“Tunawashukuru
wahudumu wa hospitali za Nyamiaga na Murgwanza, pamoja na serikali ya wilaya,
na kwa namna ya pekee wanakijiji cha Rwakalemela, waliotoa eneo la kuwahifadhi
wenzetu; Mwenyezi Mungu awabariki.” Alisema Bi. Kapaya.
Aidha,
Mkurugenzi wa Idara ya Kuwahudumia Wakimbizi Wizara ya Mambo ya Ndani hapa
Nchini Bw. Harison Mseka, alisema kwamba jumla ya wakimbizi 21,000, wamerejea
nchini Burundi kutoka kwenye kambi za wakimbizi mkoani Kigoma tangu Septemba
2017.
Alisema kila
wiki wakimbizi 2,000 wanatakiwa kurejea nchini Burundi, sawa na 8,000 kwa
mwezi, na kuongeza kwamba mwaka jana walilenga kurejesha wakimbizi 12,000,
lakini walifanikiwa kuwarejesha wakimbizi 13,300.
Bw. Mseka
alisema mwaka huu wanalenga kuwarejesha wakimbizi wapatao 80,000, ikiwa ni
utekelezaji wa makubaliano waliojiwekea kwa mwaka huu.
Amefafanua
kwamba majeruhi 26 wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Murugwanza, na
Hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza, ambapo wengine wako katika kambi ya
Lumasi.
|
Saturday, April 07, 2018
Bi. Kapaya Awashukuru Wafanyakazi wa Hospitali za Nyamiaga na Murgwanza wilayani Ngara.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment