![]() |
Wakizungumza
February 7 mchana katika mkutano wa hadhara wa kata ya Rulenge, baadhi ya
wananchi wamewataka viongozi kubainisha vipengele vilivyopendekezwa na Ngeze
vinavyobainisha kuifuta mamlaka ya mji mdogo wa Rulenge.
Katika
mkutano huo Jamadali Ruguge na Simon Nyabenda wamemtaka Mtendaji wa Halamshauri
kuwaeleza wananchi kama malaka hiyo inayo hati ya utambulisho na kutoa taarifa
ya mapato na matumizi pamoja na changamoto zilizopo kiutendaji.
Katika barua
hiyo Ngeze alifafanua kuwa vijiji vitatu vya Munjebwe Rulenge na Muyenzi
viliwekwa kuwa ndani ya Mamlaka lakini halmashauri ya wilaya ya Ngara
imeshindwa kuboresha miundombinu ya barabara maji na umeme.
Amesema
watendaji wa mammlaka wanashindwa kuendesha vikao kwa kukosa posho za wajumbe
licha ya kusanywa mapato yanayopelekwa halmashauri ya wilaya na hakuna mrejesho
wa kuendeleza miradi ya wananchi wa Rulenge.
|
![]() |
Barua hiyo
ilitaja huduma zinazotakiwa kuwa zimeboreshwa katika mamlaka hiyo iliyoanzishwa
mwaka 2015 baada ya kupendekezwa na Mbunge mstaafu wa jimbo la Ngara Deogratias
Ntukamazina ni ujenzi wa kituo cha Afya, Soko , shule nk.
Mamlaka ya
mji mdogo wa Rulenge yenye vitongoji 17 vyenye wakazi 17,826 walioko kwenye
kata moja ya Rulenge , wananchi hao wanalalamikia pia Pius Ngeze kwa kuhodhi
ardhi kubwa bila kuiendeleza wakikosa huduma za kijamii.
Ngeze
alipotafutwa kueleza malengo ya kuandika barua hiyo amekiri na kudai kuwa
Halmashauri haina budi kuifuta na kubaki serikali za vijiji ambapo viongozi
wataweza kujiwekea mipango ya maendeleo bila kuwa tegemezi.
“Mamlaka
zote duniani haziwezi kujiendesha bila fedha za kutekeleza miradi yake ambapo
mamlaka ya mji wa Rulenge ni tegemezi toka halmashauri ya wilaya na mkurugenzi
mtendaji ameshindwa kuisimamia” Amesema Ngeze.
Aidha
amesema ardhi anayolalamikiwa kuimiliki kinyume na utaratibu ni mali yake na
wanafamilia ambayo aliioomba serikali ya kijiji cha Rulenge mwaka 1984 baada ya
kuhamia kijiji hicho akitokea kijiji cha Muganza wilayani humo.
Amesema
baada ya kuibuka madai ya ardhi hiyo kutoka kwaa baadhi ya watu waliounda
kikundi cha madai ya ardhi na kufunguliwa kesi mahakama ya wilaya ya Chato na
kuwashinda baada ya kuonyesha vielelezo na nyaraka zilizotakiwa.
|
![]() |
Hata hivyo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara, Erick Nkilamachumu ( pichani ) amesema barua
aliyoandikiwa na Ngeze akipendekeza kuifuta Mamlaka ya Rulenge imepokelewa
lakini hadi kukaa vikao rasmi kupita ofisi ya Rais TAMISEMI.
Amewataka wananchi
kuvuta subira wakizubiria baadhi ya kero kama migogoro ya ardhi kutatatuliwa na
Waziri mwenye dhamana Wiliam Lukuvi anayetarajia kufanya ziara wilayani Ngara
muda mfupi ujao.
|
No comments:
Post a Comment