![]() |
|
Pichani ni Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Raila
Odinga jijini Nairobi wamekuwa barabarani wakisherehekea hatua ya Mahakama
kubatilisha Matokeo ya Uchaguzi wa Urais leo September 01,2017.
|
![]() |
|
Mgombea wa Muungano wa Nasa, Raila
Odinga.
Kufuatia Mahakama
ya Juu nchini Kenya kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi mkuu wa urais
uliofanyika mapema mwezi uliopita wa nane katika uamuzi kuhusu kesi
iliwasilishwa na muungano wa upinzani National Super Alliance ,Mgombea urais wa
upinzani Bw.Raila Odinga amesema leo
September 01,2017 ni siku ya kihistoria
kwa Kenya na kwa Afrika.
"Tulisema
tangu awali kwamba safari yetu ya Canaan haiwezi kuzuiwa. Siku ya tarehe 8
Agosti tulivuka mto Jordan."
Bw Odinga
amesema upinzani hauna imani kwamba tume ya sasa ilivyo inaweza kuandaa
uchaguzi huru na wa haki.
|

![]() |
| Wafuasi wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga jijini Nairobi wamekuwa barabarani wakisherehekea hatua ya Mahakama kubatilisha Matokeo ya Uchaguzi wa Urais leo September 01,2017. |



![]() |
|
Hii ni mara
ya kwanza katika historia ya Taifa hilo kwa Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya
uchaguzi na inaweka rekodi mpya katika historia ya uchaguzi barani Afrika ndani
ya mfumo wa vyama vingi.
Katika
uchaguzi uliopita,Bw. Odinga alienda
mahakamani kupinga matokeo lakini Mahakama hiyo ilitupilia mbali hoja zake na
kuridhia matokeo yaliyompa ushindi Rais Kenyatta.
Katika
uchaguzi wa Agosti 8,2017,Bw. Kenyatta
alitangazwa mshindi kwa kupata kura 8,203,290 sawa na asilimia 54.27, huku
mpinzani wake Bw.Odinga akipata kura
6,762,224 sawa na asilimia 44.74.
Kwa uamuzi
uliotolewa na mahakama, uchaguzi mwingine unapaswa kufanyika katika kipindi cha
siku 60. Iwapo ushindi wa Kenyatta ungeidhinishwa angepaswa kuapishwa Septemba
12.
Kumekuwa na
shamrashamra katika mitaa mbalimbali ya Nairobi na Mombasa kushangilia uamuzi
huo, huku Odinga akiwa na wanasiasa wenzake wamepongeza wakisema watatoa
taarifa zaidi baadaye.
|









No comments:
Post a Comment