|
Jeshi la
polisi kwenye Wilaya ya Karagwe limewatia mbaroni watuhumiwa waliohusika kwenye
shambulio la mikuki lililofanyika juzi dhidi ya Mkuu wa Wilaya hiyo,Bw.Godfrey
Mheruka na Diwani wa kata ya Nyakahanga Mhe.Charles Bechumila na inasemekana kuwa
washambuliaji hao ni watoto na walinzi wa aliyetoa agizo la shambulio hilo.
Kwa mujibu
wa Mkuu huyo wa Wilaya shambulio hilo linatokana na mgogoro wa ardhi uliopo
kati ya wananchi na mtu anayejulikana kwa jina la Kamiyanda ambaye
amejimilikisha ekari 152 za eneo hilo na pindi diwani alipoitisha mkutano wa
kijiji bwana huyo alihisi ni mbinu za kumtoa yeye na hivyo kuwatuma watu hao
kwa ajili ya shambulio hilo.
Diwani
Bechumila aliyejeruhiwa kutokana na tukio hilo alichomwa mikuki minne maeneo ya
shingoni, ubavuni, kifuani na kwenye paja na mpaka sasa bado anapatiwa matibabu
katika Hospitali ya Nyakahanga.
|
No comments:
Post a Comment