![]() |
|
Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, akihutubia waumini wa
kiislamu.
Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dk
Hussein Mwinyi, leo September 01,2017 amewaongoza waumini wa Kiislamu
katika kusherehekea sikukuu ya Eid El Hajj ambayo ni maarufu kama ‘Eid ya
Kuchinja’.
Waziri Mwinyi amesisitiza suala la amani kwa
Watanzania wote huku akikazia maneno ya Mufti Zuberi aliyokuwa ameyatamka ili
waumini waweze kubadilika, akimaanisha kuondokana na dhana zote potofu
zisizokuwa na manufaa katika kulijenga taifa chini ya Rais Magufuli na serikali yake.
Hafla hiyo
imefanyika jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Masjid Taqwa, Ilala-Bungoni
jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 1:30 asubuhi ambapo Sheikh wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Alhad Mussa na Mufti Mkuu wa
Tanzania, Abubakar Zuberi, na
viongozi wengine wamehudhuria sherehe hizo.
|
![]() |
|
Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zuberi
akisoma ujumbe wa Eid El Hajj kwa Watanzania.
|
![]() |
|
Baadhi ya
Waislam waliofika kwenye sherehe hizo.
Akizungumza
katika viwanja hivyo, Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zuberi amesema
kuwa anawatakia Waislamu kote nchini na wananchi kwa jumla sikukuu njema ya Eid
El Hajj ili kila mmoja aisherehekee kwa utulivu na mshikamano.
Amewataka
pia walimu kote nchini wa shule za Kiislamu za madrasa kufanya jitihada kubwa
ya kuhakikisha wanawaelimisha wanafunzi wao ili waweze kuwa na maadili mema na
si kuwapatia elimu ya dini yao tu, bali wafundishwe pia masomo mbalimbali ili
kuwawezesha kuwa na maadili mema na utaalam unaotakiwa katika maisha yao ya
baadaye na kuwa viongozi bora.
Mufti alitoa
miezi sita kwa taasisi iliyokuwa na jukumu la kuwasafirisha mahujaji kwenda
Makka na kushindwa kufanya hivyo, irudishe fedha ilizokuwa imezichangisha
kutoka kwa waumini waliotegemea kwenda huko.
Alisema
waumini hao wataweza kwenda kuhiji huko Makka mwaka kesho na kwamba uongozi
wake utahakikisha tatizo kama hilo haliwezi tena kujitokeza na kuathiri safari
za mahujaji.
|









No comments:
Post a Comment