Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 10
Januari, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Rais wa
Nigeria Profesa Ibrahim Gambari nyumbani kwake Chato Mkoani Geita.
Mazungumzo
yao yalilenga masuala mbalimbali ya uhusiano kati ya Tanzania na Nigeria.
Rais
Magufuli amempongeza Rais Muhammadu Buhari kwa jitihada kubwa anazochukua kwa
ajili ya kuleta maendeleo nchini mwake.
Pia, Rais
Magufuli amempongeza Rais Buhari kwa jitihada anazozifanya za kukabiliana na
kundi la Boko haramu ili kuhakikisha amani inaendelea kudumu nchini mwake.
Kwa upande
wake Mjumbe Maalum wa Rais wa Nigeria, Profesa Ibrahim Gambari amempongeza Rais
Magufuli kwa ushindi alioupata na jitihada anazochukua katika kupambana na
rushwa na kubana matumizi jambo ambalo linaungwa mkono na wananchi wengi wa
Nigeria.
Profesa
Gambari alimkabidhi Rais Magufuli barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Rais
Muhammadu Buhari wa Nigeria.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano,
IKULU
Chato, Geita
10 Januari, 2017
|
No comments:
Post a Comment