Taswira Picha Wananchi Bukoba leo Septemba 11,2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 11, 2016

Taswira Picha Wananchi Bukoba leo Septemba 11,2016 kwenye Uwanja wa Kaitaba.


Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa aungana na Wanabukoba leo Septemba 11,2016 kufuatia Tetemeko la ardhi  la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nchini na watu zaidi ya 10 wamekufa na wengine 120 wamejeruhiwa huku majengo mengi yakibomoka hasa ,huku Mkoani Kagera likileta matatizo makubwa kwa Wakaazi wa Manispaa ya Bukoba na Vitongoji vyake.


Katika taarifa ya Ikulu jana, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Salim Kijuu kutokana na vifo vya watu kadhaa vilivyotokea kutokana na tetemeko hilo la ardhi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

 
Katika salamu hizo, Rais Magufuli ameeleza kushitushwa na taarifa za tukio hilo lililosababisha idadi kubwa ya watu kupoteza maisha, wengine kujeruhiwa pamoja na uharibifu wa mali. Amesema anaungana na familia zote zilizopoteza ndugu, jamaa na marafiki na anawaombea marehemu wapumzishwe mahali pema peponi. Amina.

Kupitia kwako Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu na wakuu wa mikoa jirani yako iliyokumbwa na tukio hilo, natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote waliopoteza jamaa zao na nawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu,” alisema Rais Magufuli na kuwaombea wote walioumia katika tetemeko hilo wapone haraka.
 




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad