Picha zaidi Kutoka Uwanja wa Kaitaba Bukoba Ibada ya kuaga Miili ya Watu 15 waliofariki kwa Tetememko la ardhi Septemba 10,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, September 11, 2016

Picha zaidi Kutoka Uwanja wa Kaitaba Bukoba Ibada ya kuaga Miili ya Watu 15 waliofariki kwa Tetememko la ardhi Septemba 10,2016.

Pichani ni Miili ya Watu 15 waliofariki na wengine 203 kujeruhiwa  katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kufuatia  tetememko la ardhi lenye ukubwa wa vipimo vya ritcher 5.7 lililotokea  mkoani humo ikiwa katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ambapo kunafanyika ibada  ya kuaga miili  hiyo na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa aungana na Wanabukoba katika Ibada hiyo leo Septemba 11,2016.


Mkuu wa wilaya ya Bukoba Mh. Deodatus Kinawiro amesema  bado Kamati ya Ulinzi na Usalama ikishirikiana na vikosi vya uokoaji pamoja na majeshi la ulinzi na usalama vinaendelea kufanya tathmini ya uharibifu wa majengo na mali uliosababishwa na  Tetemeko hilo.

Mhe. Kinawiro ameongeza kwamba taarifa zaidi zitaendeleo kutolewa kadri zitakavyopatikana  kutokana na kuendelea kwa kazi ya  tathmini ya athari ya tetemeko hilo.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad