Spika wa Bunge la Jamahuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiingia katika ukumbi wa Bunge
kuongoza kikao cha saba cha bunge la kumi na moja leo mjini Dodoma.
Spika wa Bunge la Jmahuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha saba cha bunge
la kumi na moja ambapo pia alisema kiasi cha shilingi milioni themanini
na tano na laki tano zimechangwa kutokana na makato ya posho ya siku
moja yawabunge kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi
mkoani Kagera.
Waziri wa Habari, utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akimueleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama (MB) picha juu ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu
wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiteta jambo na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela
Kairuki wakati wa kikao cha saba cha bunge la kumi na moja leo mjini
Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo (MB) akijibu
swali bungeni ambapo alisema kuwa serikali itaendelea kupeleka fedha
katika serikali za mitaa kwa kuzingatia hali ya makusanyo ya kila mwezi.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akijibu swali bungeni ambapo
alitoa wito kwa wabunge kuisaidia kutoa elimu kwa wananchi waliovamia
maeneo ya jeshi kuondoka ili kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi baina
ya jeshi na wananchi, wakati wa kikao cha saba cha bunge la kumi na moja
leo mjini Dodoma.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Mhandisi Gerson Lwenge akijibu swali bungeni ambapo alisisitiza kuwa
Serikali inatekeleza program ya maendeleo ya Sekta ya maji kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, wakati wa kikao cha saba
cha Bunge la kumi na moja leo mjini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.
Jumanne Maghembe (MB) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula (MB), wakati wa kikao cha saba
cha Bunge la kumi na moja leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mhe.
Joseph Haule akiuliza swali bungeni kutaka kujua mikakati ya serikali
katika kutatua migogoro baina ya wakulima na wafugaji inayopelekea
mauaji ya raia ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba kwa
niaba ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi alisema Serikali
itawachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaohusika na mauaji ya
raia nchini hasa ikiwemo wanaohusika kwenye migogoro hii.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.
No comments:
Post a Comment